Mambo ya mazuri hutokea!
Kila ninapofika nyumbani kutokea shule,kitu nachopendelea kufanya ni kusubiri kipindi cha ''Nguvu ya Binti “ katika radio. Ni wakati pekee ambao mtangazaji huzungumzia mambo Fulani yanayowaathiri wasichana wadogo kama mimi na wewe.
Wiki iliyopita watangazaji walikuwa wakizungumzia kuhusu mwonekano wa mwili. Kulingana na watangazaji, mwonekano wa mwili ni mojawapo ya vitu viletavyo hofu kubwa kwa wasichana. Utafiti uliofanywa mtaani ulibaini kuwa msichana 1 kati ya 3 aliacha kupendezwa na mwonekano wa mwili wake alipofika umri wa kubalehe. Wengine walihisi si warembo vya kutosha, na wengi walihisi si wembamba vya kutosha. Hii hutokea kwa sababu wasichana wengi hawafahamu jinsi ya kumudu mabadiliko yanayotokana na kubalehe na kukua katika miili yao.
Hili lilinishangaza sana! maana siku zote Mama yangu alikuwa akiniambia ya kuwa mimi ni mzuri kwa jinsi nilivyo, lakini nadhani wasichana wengi hawakuwahi kusikia haya. Nilitaka sana kufanya kitu kuhusu hili jambo, hivyo niliwaalika marafiki zangu nyumbani kwetu baada ya shule ili kuzungumzia suala hili.
Tulikaa pamoja na kujadili hisia na maoni yetu juu ya jinsi ilivyo kwa wasichana kama sisi kukua huku tukizungukwa na watu wenye maumbo mbali mbali ya mwili ambayo ni tofauti na sisi . Tukiwa tunaongelea mabadiliko tuliyopitia kipindi cha kubalehe kilionyesha jinsi gani a,bavyo stori zetu zilifanana. Wasichana waliojiisikia wapweke huko kipindi cha nyuma wakagundua hawakuwa peke yao waliopitia hii hali ya kuipenda na kuichukia miili yao. Unaona sasa, huwezi kuwa peke yako katika jambo lolote unalolipitia. Kuongea na marafiki unao waamini kuhusu mwili wako na mabadiliko unayopitia hukufanya kujiamini zaidi.
Baada ya kumaliza maongezi yetu,tuliamua sasa tutafute suluhisho. Tukaongelea njia nzuri za kiafya za kufanya tuipende miili yetu. Na mwisho tukaweka ahadi ya kuwa hatutajilinganisha miili yetu na ya watu wengine. Miili yetu inabadilika kwa namna ya tofauti na ya pekee na wote tunapitia balehe kwahiyo ni kitu cha kawaida.
Mazungumzo haya ya baada shule sasa yamegeuka na kuwa klabu inayotambulika ya wasichana ambapo tunazingatia mazungumzo muhimu kuhusiana na balehe na mambo tunayopitia kama wasichana! Nilianza na wasichana 5 na sasa hivi wapo 50!
Tunapozungumza pamoja kama wasichana, tunafundishana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja na HAKUNA chochote chenye nguvu na kizuri kushinda hicho.
Share your feedback