Jina langu ni Debora. Nilipokuwa nakua sikuwahi kujua kuwa kutakuwa na wakati ningekuwa na msongo wa mawazo katika maisha yangu. lakini siku hizi kuna wakati nikiamka nahisi huzuni au hasira. Tendo rahisi kama kuamka kitandani naliona gumu kweli.
Nimekuja kujifunza kwamba kuwa na msongo wa mawazo ni tofauti na kuwa na huzuni. Msongo wa mawazo ni huzuni kali ambayo inaweza kukufanya uhisi kukosa matumaini, kukosa msaada na kujiona huna maana. Hali ya msongo wa mawazo inaweza kudumu muda mrefu, sio siku moja au mbili tu. Wakati mwingine kuna sababu zilizo wazi, na wakati mwingine haijulikani kwanini tunasijikia hivyo.
Msongo wa mawazo siyo kitu kizuri. Unaweza jisikia vibaya sana. Unaweza kukosa hamu ya kula, au unajisikia kulia bila sababu, ghafla unakuwa hufurahii mambo yote ambayo unapenda kufanya. Je umewahi kujisikia hivyo? Usijali ni kawaida kabisa kutojisikia sawa. Tujibebe tuna videokezo vichache ambavyo vinaweza kukusaidia kujisikia vizuri ikiwa unajisikia kuwa na msongo wa mawazo.
Usijisikie vibaya: jambo la kwanza unalohitaji kujua ni kwamba ni kawaida kutojisikia sawa nyakati nyingine. Usijaribu kujitenga na wengine kwasababu watu wengiwanakabiliwa na msongo wa mawazo na wanaweza kukusaidia.
Jaribu kujenga mawazo chanya: Msongo wa mawazo haukufanyi ujisikie vibaya tu bali hata kuwa na mawazo hasi juu yako mwenyewe. Mawazo kama "Mimi ni wakushindwa tu", "Hakuna mtu anayenipenda" au "Mimi sio mzuri" yanaweza kuzunguka akili zetu. Lakini kama tunajaribu kuanza kufikiri vizuri kuhusu sisi wenyewe kwa kuwaza mazuri mfano; "Mimi ni wa kipekee, mimi ni imara, mimi ni mkarimu, nina upendo" inaweza kutusaidia kukabiliana mawazo hasi.
Kuongea juu ya tatizo lako ni sehemu ya utatuzi: Ikiwa unajiona huna matumaini au uchovu au ikiwa unapoteza hamu ya vitu au kujiona upo gizani au mambo ni magumu, na ni vigumu kukabiliana nayo. Ni muhimu kutafuta mtu unayemuamini kama mwalimu, rafiki bora au wazazi na kuzungumza naye. Utaona inasaidia kuongea na mtu juu ya hisia zako. Inawezekana kabisa wakapata ugumu wa kuelewa hisia zako, hivyo tumia muda wa kutosha kujaribu kuwaelezea. Kumbuka kama unahisi haueleweki, hiyo pia ni sawa -binadamu tuko tofauti na baadhi ya watu wanaweza kushindwa kuoanisha unachokisema, hilo lisikufanye ujihisi kuwa unakosa. Kutoeleweka hakukufanyi uwe na kosa.
Zoezi kidogo husaidia: kufanya mazoezi husababisha vichocheo vya furaha yaani endorphins kuachiliwa mwilini, homoni hizi zinatusaidia kujenga hisia bora kiakili na kimwili. Kujiunga na timu ya michezo shuleni au katika jamii yetu inasaidia, kuongeza mudi na kujisikia vizuri zaidi.
Share your feedback