Wavulana hubalehe pia
Kubalehe ni jambo ambalo sote hulipitia. Inaweza kuwa safari yenye changamoto na unaweza kujisikia kama unaipitia pekeako, lakini haipaswi kuwa hivyo.
Kuzungumza na watu walio karibu yako kuhusu mambo kama vile hedhi na mabadiliko ya hisia inaweza kukusaidia kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko unayoyapitia. Lakini pia ni njia nzuri ya kutoa na kushirikisha ushauri.
Wakati mwingine hatujisikii huru kuzungumza na wavulana kuhusu ubalehe kama vile tunavyozungumza na wasichana wenzetu, Mara nyingi hii inasababishwa na dhana potofu kuhusu vile wanavyotuchukulia.
Basi Wasichana, tupo hapa kuziondoa dhana hizo.
Dhana 1 – miili ya wavulana haipati mabadiliko
Kwa sababu wavulana hawapati hedhi hii haimaanishi kwamba hawapitii uzoefu wa kubalehe. Kama ilivyo kwetu miili yao pia hupitia mabadiliko kadha wa kadha. Kwa mfano, Je hivi unafahamu ni katika kipindi hiki ndipo wavulana huwaanza kuota nywele kwenye maeneo yote ya miili yao na sauti zao huwa nzito?
Dhana 2 – wavulana hawafahamu chochote kuhusu wasichana
Hii si kweli, lakini kama una rafiki au ndugu wa kiume ambao hawaelewi unachokipitia, waambie! Jitayarishe kwani huenda wakawa na maswali mengi sana - jibu yale ambayo unajisikia huru kuyajibu tu!
Dhana 3 – wavulana hawajali kile tunachokipitia
Wavulana wanaweza kutusikiliza vizuri mno na wanajali sana maisha yetu kuliko tunavyofikiri. Ingawa wakati mwingine huenda usihisi hivyo, ila wanajali kuhusu kile tunachopitia.
Kubalehe kunaweza kukawa kipindi kigumu sana, lakini kadri tunavyozungumza kwa uwazi zaidi ndivyo ambavyo marafiki zetu wa karibu watakavyoendelea kutuelewa zaidi.
Kuwa waaminifu na wawazi Kati yetu itatufanya tujifunze zaidi. Kubalehe haipaswi kuwa kitu cha kukiogopa kwa sababu wote tunakipitia.
Share your feedback