Kuwa msichana ninayejitegemea –sehemu ya 1

Inaanza na wewe

Mambo vipi msichana, Jina langu ni Tanya, Nina miaka 17 na nilitamani sana kuwa na maisha huru na ya kujitegemea. Niliishi maisha mazuri. Nilienda shule, Mara zote nilikuwa na chakula na nguo za kuvaa, lakini kipindi baba alipopoteza kazi maisha yalibadilika sana na kuwa ya hovyo. Ilinibidi niache shule kwani alishindwa kumudu kunilipia ada.

Swala la kuacha shule lilikuwa ngumu. Nilihisi ingenifanya niachane na ndoto za kuishi maisha ya kujitegemea, kwa sababu bila ya kuwa na elimu nilihisi isingekuwa rahisi kutimiza ndoto zangu. Siku moja nikiwa chumbani nilikuwa nikisoma baadhi ya stori katika ukurasa wa Springster nilipobonyeza sehemu iliyoandikwa kuwa bosi wa maisha yako. Hiki ndicho kitu nilichokuwa nakitaka hasa kusoma katika kipindi kile.

Kupitia stori hizi nilijifunza kuwa naweza kuanzisha biashara na kuwa mwenye kujitegemea. Elimu haikuwa njia pekee. Lakini ili niweze kuianza safari hii niliopaswa kubadili mtazamo na jinsi nilivyosikia.

Hatua ya kwanza katika kuelekea kuwa msichana unayejitegemea ni kujiamini na kuamini uwezo ulionao katika kutimiza ndoto zako. Nafahamu kuwa Mara nyingine ni vigumu kujiamini hasa pale kila kitu kinachokuzunguka kinaonekana kwenda kombo, lakini usijikite katika hayo. Badala yake kuna mambo mawili unayoweza kuyafanya.

Kuwa na mawazo chanya

Wanasayansi wanasema karibu asilimia 70% ya mawazo yetu huwa ni mawazo hasi. Je ulilijua hili? Na bibi yangu Mara zote amekuwa akiniambia kuwa " mawazo hasi hayawezi kukupa maisha chanya" amesema ukweli mtupu. Ili uweze kujitegemea unapaswa kuondoa mawazo hasi na kuboresha mawazo chanya.

Tambua ujuzi na vipaji vyako

Nilikuwa nikifanya vizuri sana nilipokuwa shule, lakini haimaanishi kwa sababu niliacha shule basi sina akili tena. Kama nilikuwa nafanya vizuri katika somo la hesabu basi naweza kufanya vizuri mahesabu ya biashara. Ni jambo la muhimu kufahamu kitu gani unakimudu vizuri. Hii itakufanya ujiamini.

Mara zote unatakiwa kukumbuka kuwa mawazo hupelekea kutengenezwa kwa hisia na hisia zako hupelekea maamuzi unayoyafanya na hatua unazozichukua. Hivyo kabla hujaweza kujitegemea unapaswa kwanza kuamini inawezekana kwako. Na unajua nini msichana? Hakika inawezekana.

Shuka chini ili uendelee kufuatilia safari yangu hii ya kuwa huru na mwenye kujitegemea sehemu ya 2. Au andika Kuwa msichana ninayejitegemea – sehemu ya 2. Hapo katika kitufe cha kutafutia.

Share your feedback