Kuwa msichana ninayejitegemea – sehemu ya 3

Usisafiri pekee yako

Mambo msichana,

Nimekuwa nikiwashirikisha kuhusu safari yangu ya kuwa msichana ninayejitegemea. Sina uhakika kama umeona stori zangu zingine lakini nilikuwa na mpango wa kuanzisha biashara ya kuoka kabla sijapata majanga. Nenda sehemu iliyoandikwa "Pia unaunaweza kupenda" uweze kusoma sehemu ya pili ili kujua nini kilitokea.

Baada ya kupatwa na janga, sikutaka kukata tamaa kwa sababu nilijiamini na nilikuwa na mawazo chanya kuhusu swala hili. Badala ya kukata tamaa niliamua kufurahia na kupiga picha na vitu vyangu vya kuokea nilivyoviweka sakafuni na kisha nikaweka picha hizo kwenye ukurasa wangu wa mtandao wa kijamii. Na kuandika hivi " nahitaji kuoka keki 50 hapo kesho ila sikuwa na mahitaji yakutosha#tumamsaada"

Mpaka muda nilipofika nyumbani, nilikuwa nimepokea meseji nyingi sana kutoka kwa marafiki na majirani kwamba Wana unga wa ziada, siagi, maziwa na sukari! Ni furaha iliyoje? Hivyo walikuja nyumbani kwetu na kunipatia mahitaji hayo na kunisaidia kuandaa kila kitu nilichokihitaji kwa ajili ya kuoka keki za kuuza kesho yake.

Ninapolitafakari hili hivi sasa... Ningefanyaje pasipo kuwa na msaada wa marafiki zangu? Nilikuwa nikidhani kujitegemea kulimaanisha kufanya kila kitu mwenyewe lakini hii haina ukweli wowote ule. Kufanya kazi kwa pamoja kama timu ndio siri kuu ya maisha. Kama nilivyosema hapo awali, safari ya kuwa huru kujitegemea ni safari yenye milima mingi, hivyo unahitaji marafiki wenye upendo na wenye kukuunga mkono katika kila hatua unayoipiga. Haupaswi kuhisi kwamba kuomba msaada kutoka kwa watu wengine ni kuwapa mzigo. Haupaswi kuishi maisha yako pekee yako.

  1. Hivyo unapoianza safari yako ya kuwa huru na mwenye kujitegeme kumbuka.

  2. Penda na amini mambo mema uliyonayo hata pale mambo yanapokuwa magumu... USIKATE TAMAA.

  3. Usijari kufanya kila kitu pekee yako. Tafuta marafiki na Familia wakuunge mkono pale unapouhitaji. Na hili halimaanishi kwamba haujitegemei.

Mwisho nilipata keki zangu 50 zilizokuwa nazihitaji niliziandaa tayari kuanza kuziuza. Nilipata pesa kidogo kwa mara ya kwanza na nilijisikia vizuri. Ilinichukua muda kufikia hatua hii ila nilijifunza mengi sana binafsi na Nina hasa maana ya kujitegemea.

Share your feedback