Wazo dogo limekua kitu kikubwa
Kwa jina naitwa Paulo naishi mji mdogo ambao una wajasiriamali wengi wanaoendesha biashara ndogondogo.Mfanyabiashara mmoja ninaemfahamu vizuri ambae huwa nanunua mbogamboga kwake ni Boke,
Miaka kadhaa iliopita Boke alinambia alikua na hofu kwakua msambazaji aliekuwa anamletea mzigo alikua anaacha na hii ingetikisa sana biashara yake.kwa kua nafahamu fika familia yake inamtegemea kulingana na kipato anachoingiza.Binafsi niliamua kulishugulikia jambo hilo.
Kwanza nikaanza kuwauliza wafanyabiashara mmoja baada ya mwingine kuhusu wasambazaji wanaowaletea mizigo.Nikaweza kupata idadi ya wakulima katika eneo letu.Nikamuomba baba yangu kama naweza kuwasiliana na hao wakulima kama watakua tayari kunipa ujuzi wa kulima mbogamboga.
Baba alinipa mbinu nitakazotumia kuwashawishi wakulima. Aliniambia nijielezee kwanini nahitaji ushauri wao. Nilimuelezea ya kuwa nilikua nawaza kulima mbogamboga mwenyewe ili niweze kumsaidia Boke na familia yangu. Mkulima mmoja alijitokeza na kunifundisha vizuri jinsi ya kulima na kukuza mbogamboga.Aliniambia kwanini utumiaji wa ardhi yenye rutuba ni muhimu,pia jinsi ya upandaji mbogamboga,jinsi ya kuzuia wadudu na muda sahihi wa kuvuna. Nilianza kidogo upandaji na nilimwambia Boke kuhusu mkakati wangu na kwamba nategemea kukuza hizi mboga ili niwe nampelekea mzigo.
Nilipoanza nilikua na mboga kidogo kwa matumizi ya nyumbani na kuuza kwa marafiki na majirani mtaani, lakini shamba langu lilivyoanza kuchipua vizuri habari zikaenea nikajikuta naongeza idadi ya wateja. Hii ilinipa fursa na kuanza kuwauzia wajasiriamali wadogo wadogo kama Boke ili waendelee kukuza biashara.
Kitu kizuri ni kwamba Boke anauzoefu wa kutosha kwenye hii biashara ya mbogamboga na alinipa ushauri wa jinsi ya kuendesha biashara yangu pamoja na mapato.Kwakua sikuwaza au hata kutilia maanani vitu vingi katika biashara yangu hii mpya ya mbogamboga nilifurahi na kushukuru mno kwa ushauri huu wa Boke.
Leo nasambaza kwa wafanyabiashara wadogo wanaouza kwa watu kwenye soko la mjini hapa kwetu na wote tunafaidika kupitia mfumo huu.
Kama una wazo kubwa au changa chukua nafasi kumuuliza mtu unaeona anafaa kuwa msaada kwako na kama unaogopa au unaona aibu jaribu kuandika malengo yako na kwamba utayafikiaje?.Chukua hatua fuata ndoto yako! Unaweza usifanikiwe kwa mtu wa kwanza uliemuomba msaada lakini usikate tamaa kwa kua mimi sikufikiria kama nitajifunza vingi kupitia kwa mkulima au Boke lakini nimepata somo moja kwamba sio lazima kwenda mbali kumpata mshauri mzuri wa kukuelekeza.
Share your feedback