Wakati kila mtu anapogundua mwili wako unabadilika
Kaka kwaheri! Ndivyo nilivyomwambia alipojaribu kunisemesha baada ya miaka kadhaa. Je, ungetaka kujua sababu? Endelea kusoma.
Nilisikia vitu vingi kuhusu ubalehe nilipokuwa ninakua. Mwili unabadilika, unaanza hedhi, homoni zinaongezeka na vitu kama hivyo. Lakini hakuna mtu aliyenijuza kuwa wavulana wataanza kuniangalia angalia. ndio maana nataka kukushirikisha stori yangu.
Kulikuwa na huyu kaka mtaani kwetu anaitwa Zain. Nilitamani sana kuwa demu wake kwa miaka mingi, lakini ndo kwanza alikuwa hata haniangalii. na mimi. Nilijaribu kuongea nae na yeye mara kadhaa, lakini alikuwa akikatisha mazungumzo na hata kujifanya hanielewi . Hii ilikuwa ni ishara kuwa hanitaki . Nikaona nimpotezee niendelee na maisha yangu.
Mwaka jana, niliongezeka sana ukubwa. Nilianza kuona matiti yangu yakiwa makubwa, hipsi zilianza kuonekana na makalio pia! Lakini sikuwa mimi pekee yangu niliyekuwa naona haya mabadiliko . Baada ya kunipotezea miaka mingi , Zain alianza kunisalimia tena. Kwanza ilikuwa “mambo” kisha akaanza kusema jinsi nilivyokuwa “Mdada” sasa nilikuwa naonekana mrembo. Akaanza kujaribu kuniambia hata nisiende shule, niwe naye, lakini sikutaka. Lakini hakuwa peke yake. Ni kama kila mtu alitaka kuniambia jinsi mwili wangu ulivyokuwa unabadilika.
Ni kweli, naweza kuwa nimekuwa Mdada sasa, lakini pia mimi ni mjanja na nina ndoto kubwa. Sikuwa tayari kuruhusu anichanganye nisifikie malengo yangu. Hasa nilipofikiria nia yake haikuwa ya kweli. Nilimwambia, Kaka - kwa heri!
Sikua na mtu wa kuongea naye nilipokuwa napitia haya, hivyo nikasema lazima niwashirikishe mdogo wangu na marafiki zake ili wapate ezoefu..
Unapo ongea kuhusu mabadiliko unayopitia na kuwapa stori yako huwa inakusaidia sana na ni faida kwako na kwa wanaokusikiliza .sasa hivi kwa vile mdogo wangu rafiki zake wanajua zaidi, wanaweza kufanya maamuzi bora. Hivo ninapogundua kitu kunihusu na katika mwili wangu, sina shida kueleza wengine ikiwa najua kitawasaidia pia!
Share your feedback