Ushauri kutoka kwa rafiki yangu wa dhati wa kiume.
Nilipokuwa kijana wasichana wengine shuleni waliniambia kwamba wavulana ni wabaya na ni lazima nikae mbali nao. Walisema kwamba wavulana na wasichana hawawezi kuwa marafiki. Ningewasikiliza lakini moyoni nilijua sio kweli.
Nina rafiki wa dhati wa kiume anayeitwa Kofi. Tumekuwa marafiki tangu utotoni. Mama zetu ni marafiki na tulizaliwa siku moja. Yeye amekuwa akinichukulia kawaida. Haikujalisha kama mimi ni msichana au la. Sisi sote tunapenda mambo yanayofanana. Sisi sote tunapenda mpira wa miguu. Sote wawili tunapenda mboga zetu. Sisi sote tunapenda kusoma vichekesho. Ningeweza kuendelea.
Hata hivyo tulipoanza shule ya upili, kijana mwenye umri zaidi yangu alivutiwa na mimi. Alikuwa akijaribu daima kuzungumza nami kwenye korido lakini nilikuwa na aibu. Aliendelea kujaribu kuzungumza na mimi mpaka hatimaye nilikubali. Tulipoanza kuzungumza mambo yalienda vizuri mpaka ghafla alipoacha kuzungumza nami. Siku iliyofuata nikamwona akitembea na msichana mwingine.
Nilihuzunika sana, nilidhalilika sana kana kwamba kuna kitu kibaya kwangu. Nilimwomba Kofi ushauri juu ya nitakachofanya maana alikuwa mvulana.
Kofi alinikumbusha kwamba hakuna kitu kibaya kwangu. Alisema thamani yangu haikutegemea na iwapo mvulana alinipenda au la. Thamani yangu inatoka ndani yangu na hakuna anayeweza kuiondoa.
Pia aliniambia nisivunjike moyo. Iwapo mienendo ya mvulana haieleweki kwangu, haina uhusiano na mimi bali inahusiana na yeye mwenyewe na mashaka yake.
Sasa ninatambua jinsi gani mimi ni wa pekee. Pia ninafahamu kuwa mvulana yeyote atakayenipenda ataniheshimu. Hatajaribu kuniaibisha au kutaka kuwahisha mambo. Ninawashukuru sana marafiki wa dhati wa kiume kama Kofi. Hii inathibitisha kwamba wavulana wanaweza kuwa marafiki wazuri na kukupa ushauri wa muhimu sana.
Share your feedback