Jinsi ya kujua ishara.
Huwa unakosa usingizi ukimuwaza mtu fulani? Je huwa unajiuliza ikiwa yeye huwa anakuwaza pia? Sote tumepitia hapo. Na ni kawaida sana kuwaza kuhusu wakaka tunapoendelea kuwa wakubwa. Hii ni sehemu ya ubalehe na utu mzima.
Kama rafiki yangu Sarah. Alimpenda kaka mmoja aliyekuwa anaitwa KB Lakini aliogopa kuwa wa kwanza kumsemesha. Sarah ni aina ya watu ambao hutaka kuhakikisha mambo kabla ya kufanya jambo lolote. Mara ya mwisho walipoongea na KB, Sarah ni alikuwa amedata kwa KB lakini bado alimuomba ushauri Dada yake ili kuwa na uhakika zaidi..
Haya hapa ni mazungumzo kati ya Sarah na KB:
KB - Wow! Sarah, umebadilisha mtindo wako wa nywele, Nimependa hizi rasta ulizosuka. Tena nimependa zaidi zile yeboyebo ulizokuwa umesuka.
Sarah – Asante! Siku nyingi sijakuona.
KB – Ndio, Imekuwa muda mrefu. Nilimwambia mshikaji wangu jana kuhusu wewe. Na pia vile jinsi ambavyo huwa nakumiss .
Sarah – Oh vizuri kusikia hivyo.. Una na mishe gani?
KB – Sina. Ninacheki ile series uliyoniambia. Naipenda! vipi unaweza kuja tucheki wote kwa pamoja?
Baada ya Sarah kumuambia dada yake hayo mazungumzo dadake akamweleza namna gani ya kujua kama mkaka anakupenda au la. Alisema hivi:
Kutokana na ushauri a huu kutoka kwa dadake, Sarah akaamua kumweleza KB alivyokuwa anajisikia na kwa bahati nzuri, KB akasema na yeye anajisikia hivyo hivyo, Weraaa!!! Wapendanao Sarah na KB!
Hata kama huna dada kama Sarah, unaweza kuongea na wasichana wengine katika jamii unayoishi kama una swali lolote!
Share your feedback