Kukabiliana na uonevu

Nilijifunza kuwa na msimamo

Mwanafunzi mwenzangu aitwaye Faridah, alikuwa akionewa Mara kwa mara. Wasichana waliokuwa wakisoma madarasa ya juu walikuwa wakimtania bila sababu yoyote. Walisabambaza vikaratasi vilivyokuwa vikimdharilisha na kuweka vitu vinavyonuka katika begi lake ama kumzodoa alipokuwa katika michezo.

Ingawa mimi na marafiki zangu wengine tulikuwa tukishuhudia na tulitamani kuzuia isitokee ila tulikuwa tukiogopa. Hatukutaka waanze kutufuatilia na sisi.

Lakini siku ambapo mmoja wa marafiki zangu alinipatia jarida kutoka Springster lililozungumzia namna ya kujitetea, tulipolisoma lilitupa ujasiri mkubwa. Hii ilinifanya nimfikirie Faridah, na niliona labda aliogopa kujitetea. Naamini hakuna anayestahili kuonewa, najua uonevu ni Kosa.

Na niliwaambia marafiki zangu kama nitawaona wale wasichana wakimuonea tena Faridah, nitamtetea. Nilikuwa na hofu ila niliamini marafiki zangu wataniunga mkono kama ningehitaji msaada. Kesho yake tulipokuwa darasani, wasichana wawili walianza kusambana vikaratasi vilivyokuwa vinamdhalilisha Faridah, na kiliponifikia hicho kikaratasi nilitaka kumsaidia, hivyo nilisimama na kwenda mbele alipokuwa mwalimu na kumwambia.

Nilimwambia "samahani mwalimu Oku, nimepokea kikaratasi chenye maneno mabaya kuhusu mmoja wa wanafunzi wenzangu. Nadhani huu ni uonevu na sio kitu sahihi. Ninaomba tusaidiane kwa pamoja kuikomesha tabia hii."

Mwalimu Oku pamoja na wazazi wa wale wasichana waonevu walikaa chini kuzungumza na aliwaambia jinsi uonevu ulivyokuwa hatari. Faridah alishukuru mno, na alianza kuwa na amani tena. Toka siku Ile mwalimu Oku aliniomba niwe muwakilishi wa kupambana na uonevu shuleni, na nilikuwa nikiongea katika matukio mbalimbali ya shule na niliwafundisha mbinu za namna ya kupambana na uonevu.

Niliwafundisha wanafunzi wenzangu namna wanavyoweza kutoa taarifa za uonevu kwa watu wazima wanaowaamini. Na wasijiweke katika hatari za kupambana na waonevu, waombe marafiki zako wakusaidie usipambane pekee yako. Na kitu cha msingi zaidi ni kwamba una nguvu ya kuikomesha tabia hii. Sauti ya mtu mmoja inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu wengine. Simama leo jiamini!

Share your feedback