Kutoka mwana mieleka wa mtaani hadi bingwa wa dunia

Kutana na wasichana wa Senegali ambao wameweka historia!

Wazazi wangu walifariki nilipokuwa mdogo, hivyo nililelewa na kinamama mtaani kwangu. Japokuwa walikuwa wananionyesha upendo mwingi, nilihama nyumba moja hadi nyingine na bado sikuhisi kama naridhika. lakini nikawa nimeanza kufanya mieleka na maisha yangu yakabadilika. Hatimaye nikawa nimepata kitu ambacho naweza kusema kuwa ni changu.

Mwanamke mmoja wa maana sana kijijini kwangu alianza mieleka Senegali miaka michache iliyopita, wakati mieleka haikuonekana kama "mchezo wa wanawake". Sambuu alivinja imani zote za kibaguzi . Alivunja miiko yote.Katika nyakati ambazo watu walidhani mieleka ni ya wanaume pekee, Sambuu aliingia uwanjani na kumshangaza kila mtu. Aliweza hata kufuzu kushiriki katika Olimpiki! Ajabu sana ... mwanamke kutoka kijiji changu kidogo nchini Senegali akishindana kimataifa. Chochote kinawezekana unapokizingatia, Unaonaje?

Isabela Sambuu aliporudi Senegali alianzisha klabu ya mieleka kwa wasichana wadogo, kwasababu aliamini kuwa wasichana wanaomfuatilia wana uwezo wa kuwa mabingwa wa dunia pia. Na hivyo ndivyo nilianza kushiriki. Nilijisajili kupata mafunzo kwa hisani ya Sambuu,maana nina ndoto kuwa siku moja nitakuwa bingwa wa dunia. Mbali na ndoto yangu, napenda mieleka kwa sababu hunifanya kujihisi mwenye nguvu na wa thamani. Unahitaji kujifunza jinsi ya kujiamini na kuamini nafsi yako, vinginevyo mpinzani wako atagundua hofu yako na unaweza kupoteza shindano.

Sambuu hakupata ubingwa kwa usiku moja. Alianzia mtaani na kuendelea hadi kufika kileleni. Nami nafanya hivyo pia ,Kuogopa ndoto kubwa haitanisaidia kwa namna yoyote, hivyo nitazingatia mafunzo kwa bidii kwa kadri navyoweza. Pia kila asubuhi ninapoamka nafumba macho yangu halafu navuta picha kama mshindi wa kila shindano na kushika medali ya dhahabu. Baada ya kuwaza kama mshindi kwa mara nyingi, sasa hivi haionekani tena kuwa ni kitu kisichowezekana.

Isabela Sambuu alikifanya kijiji chetu tujivune, hadi wazee wakamfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa chifu na kiongozi kijijini. Na kwa sababu sasa nimegundua kwamba ndondi ndicho kitu ninachokitaka kufanya maishani, nitakifanya kwa kila namna niwezayo. Sitaacha kuchukua hatua na kufuata ndoto zangu kwasababu wasichana wanapoingia ndani ya ulingo, mambo makubwa yanaweza kutendeka!

Je unataka, kuvunja rekodi kwa kufanya kitu cha tofauti maishani mwako? tuambie hapo chini kwenye sehemu ya maoni kuhusu mipango yako,unachotakiwa kufanya ni kujisajili tu.

Share your feedback