Rafiki yangu kipenzi alinisaidia kuamini vipaji vyangu
"Msaada unahitajika kwenye tamasha la uigizaji: tunahitaji mtaalamu wa Kupamba )."
Tumbo langu lilitetemeka niliposoma lile tangazo. Nilijisikia uoga, lakini nilitamani kuwasaidia. Nilikuwa nikipenda sana darasa la Sanaa, na nilikuwa mchoraji mzuri sana, lakini Je ningeweza kuremba watu kweli? Kuwa kama mtaalamu wa kupamba watu katika tamasha hili la shule lilikuwa jambo kubwa kwangu. Hili lilikuwa tukio kubwa mno pale shuleni. Ila sasa naogopa nikikosea itakuwaje? Kuwa mchoraji katika darasa la Sanaa ilikuwa kitu tofauti ,na kumpamba tu lilikuwa jambo jingine kabisa. Jambo hili lilinitia uoga kiasi.
Nilikuwa nimejisahahau mpaka pale rafiki yangu kipenzi Lulu - ambaye alikuwa mhusika mkuu wa kike katika igizo alipokuja nyuma yangu.
"Rehema unawaza nini aliuliza kwa sauti yenye uchangamfu mkubwa.
"Oh hapana," nilidanganya, lakini Lulu alikuwa ananijua vizuri mno.
"Nafahamu unawaza nini maana unachosema haikiendani na sura yako... Wewe unawaza wewe tena sana."
"Mmh ni kweli! nilishikwa na kigugumizi." Nina wazo moja zuri. Naona nahisi kusaidia kuremba watu kwa ajili ya igizo."
"Wao!, Rehema. Hii imekaa poa sana hii " Lulu kidogo apige kelele. Aliniambia mimi nilikuwa mmojawapo wa wasanii wazuri mno aliokuwa akiwafahamu na kwamba angependa nihusike vilivyo.
"Naomba uje nyumbani kwetu mara tu baada ya kutoka shule, nitawakusanya baadhi ya waigizaji pamoja. Uje vipodozi vyako vya kupambia na mie nitamuomba mama yangu kama anaweza kuturuhusu kutumia baadhi ya vipodozi vyake. Mimi nakuaminia Rehema. Unaweza!"
Nilipokuwa nikitembea kuelekea nyumbani kwa akina Lulu. Nilijawa na uoga na nilitamani nisingekuwa nimekubaliana na huu mpango hata hivyo, nilipofika niliwakuta waigizaji watatu wakiningojea, na walikuwa na sura zenye tabasamu. Nisingeweza kurudi nyuma tena. Rafiki yangu aitwaye Edwin alinionyesha meza ndogo iliyokuwa imeandaliwa na juu ya hii meza palikuwa na maandishi yaliyosomeka ”Studio ya "make up" ya Rehema."
Waigizaji mmoja baada ya mwingine, walipata nafasi ya kunionyesha picha ya mitindo ambayo walitaka niwarembe na ndipo nikaanza kuwachora. Na siku hiyo nilimchora mmoja wa wavulana akafanana na simba, nilimgeuza Lulu akawa kama malkia , na nilifanya ma utaalamu yangu na kumgeuza mmoja waigizaji akafanana kama mchawi anayetisha Nilifurahi mno mpaka nilisahau hata kama hapo mwanzo nilikuwa naogopa.
Hii ndio ilikuwa siku ambayo marafiki zangu waliniamini sana na ikanifanya nianze kujiamini mwenyewe pia. Nawashukuru sana marafiki zangu kwani nimethubutu kuzifuata ndoto zangu
Haya Jamani Rehema kafanikiwa Je una kipaji ambacho umeanza kukifanyia kazi kama Rehema? , tunaomba utuambie stori yako kwenye sehemu ya maoni hapo chini.Tunapenda sana kusikia kutoka kwako.
Share your feedback