Na nikabakia kwenye shuleni Yangu!
Wiki kadhaa zilizopita wazazi wangu walinikalisha chini na kuniambia walitaka kunihamishia kwenye shule iliyokuwa mbali na nyumbani- ambayo ni shule ya bweni. Nilipatwa na mshangao mkubwa, sikujua hata niwaambie nini.
Sababu iliyowafanya wafikie maamuzi haya ni kutokana na kuwa baba na mama hushinda kazini siku nzima na kwa hiyo wakajawa na wasiwasi ya kuwa hakutakuwa na mtu wa kunisimamia kwenye kazi zangu za shule. Hivyo kama ningepata shule ya bweni ingenisaidia kuzingatia masomo yangu vizuri na kupata muda mwingi wa kujisomea.
Nilishituka na nilifikiria sana, nikajiuliza (hivi wanawezaje kunifanyia hivi?) kwa (hasira tulibishana sana,) nilikuwa na huzuni (kwani sikutamani kuwa mbali na nyumbani) lakini pia niliogopa (Je nitawezaje kujitegemea bila kuwa na msaada wa mtu yoyote?)
Baadae nikagundua kuwa hili wimbi la mawazo halitanisadia chochote. Hivyo nikakaa chini na kuandika sababu zilizonifanya kutokukubaliana na uamuzi wao, na jinsi ntakavyoweza kufanya vizuri ikiwa ntabakia nyumbani huku nikienda katika shule niliyokuwa nikisoma.
Niliwapelekea wazazi wangu hii orodha, na tulizungumza kwa muda mrefu, (Na wakati huu hatukuwa tukirumbana), Huku nikiwaonyesha faida na hasara, niliwaeleza kwamba najisikia mwenye furaha mno kuwepo katika shule niliyopo, na hata matokeo yangu ni mazuri, lakini pia nina marafiki ambao niliwapenda na kuwathamini sana. Niliwaomba waendelee kuniamini na nikawa ahidi nitafanya vizuri shuleni, hata kama watakuwa wakichelewa kurudi kutoka kazini. Wazazi wangu walifurahi mno namna nilivyoweza kujieleza na kutatua tatizo. Waliridhika na mawazo yangu. Waliniona nimekuwa na ninaweza kusimamia kile ninachokiamini kuwa ni sahihi, na waliniamini zaidi.
Na tulikubaliana kwamba hawatanipeleka katika shule ya bweni, na ikitokea mama na baba watabanwa sana na kazi tutakaa tena tujadiliane nini cha kufanya.
Hivyo basi, siku ambayo utatofautiana au kutokukubaliana kitu ambacho wazazi wako au walezi wako wamekiamua, kumbuka kwamba unahaki ya kuwaambia mtazamo wako. Ikiwa utakabiliana na hiyo hali kwa utulivu, na kwa ujasiri ni wazi kwamba watasikiliza maoni yako.
Share your feedback