Nafaa kuwa na marafiki wangapi?

Thamani ni kitu bora kuliko Wingi!

Mambo Vipi!

Jina langu naitwa Taiba. Wakati nilipoenda sekondari, kuwa na kundi la mashosti ilikuwa ndo mpando mzima. Yaani Kama hukuwa na “kikundi” basi ulionekana wa ajabu kwelikweli.

Niliwaona watu wengi wakiwa wakiishi maisha feki na wakifanya mambo wasiyoyataka kwa sababu walihisi wasipofanya hivyo watapigwa chini na mashosti.

Lakini niko hapa kukuambia kwamba urafiki haimanishi uwingi, bali ni ile thamani ya urafiki. Ina haja gani kuwa na marafiki 10 ikiwa hakuna hata mmoja atakayekuja kwenye bethidei yako? Au hakuna hata mmoja atakaekuwa bega kwa bega na wewe wakati wa matatizo.

Najua wakati mwingine huwa tunawaza sasa watanionaje?, au ntaonekanaje? Lakini kuishi maisha yako kutokana na jinsi ulivyo hata kama utakuwa peke yako ni bora zaidi,niamini mimi nakwambia.

Unapokuwa unaishi maisha yako utawavuta tu wale ambao ni marafiki wa kweli watakaokupenda wewe kwa jinsi ulivyo. Sio wale marafiki wanaotaka tu wakutumie kwa mambo yao. Kama rafiki yangu Jeni. Yeye ni rafiki yangu wa dhati na wa pekee sana, na ninafurahi sana kuwa naye maishani mwangu. Huwa yuko tayari kunisaidia ninapomhitaji. Hunisaidia hata na kazi za shule, na huwa tunaenda nyumbani pamoja, Licha ya hayo huwa tunalindana sana. Yaani yeye huninunulia hata chochote kama zawadi anapoenda mjini. Sasa huyo ndio rafiki wa kweli. Huwa hanipigii simu tu pale anapokuwa na shida. Au kunionyesha kuwa ana hela.Huwa yuko mimi wakati wa shida na raha! yaan kila mtu anamjua mwenzake vizuri.

Siwezi kwamwe kumfananisha Jeni na marafiki wengine. Yeye peke yake tu ni sawa na marafiki milioni moja! Na ninampenda mno.

Kwa hiyo Jamani, usizingatie idadi ya marafiki ulionao... Zingatia aina ya marafiki ulionao, na hakikisha ni wazuri!

Share your feedback