Nimeishiwa Pedi…

Na sina pesa za kununua zingine

Mambo vipi wasichana!

Jina langu naitwa Naobi. Wiki iliyopita nilitingwa sana. Nilikuwa nikisoma kwa bidii ili kujiandaa na mitihani yangu ya mwisho. Nilikuwa na hofu sana, sikutaka kutokufaulu na kushindwa kwenda kwenye darasa lililofuata.

Ijumaa asubuhi, niliamka nikiwa mwenye furaha, nikiwa nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mitihani yangu mwili ya mwisho. Nilipiga mswaki, kunawa uso na kisha kuoga. Wakati nikiwa naoga niligundua kuwa nilikuwa nimeanza hedhi.

Niliangalia kwenye mkoba wangu na kugundua nilikuwa nimeishiwa pedi. Nikaangalia kwenye boksi nililokuwa nikitunzia pesa lakini sikuwa na pesa ya kutosha kununua pedi mpya. Badala yake nilitumia kitambaa kisafi na kuvaa chupi mbili kisha nikaenda shule.

Nilifanikiwa kumaliza mitihani wangu wa kwanza vizuri. Lakini ilipofika mchana, damu ilikuwa ikitoka nyingi na kile kitambaa hakikuweza kunisaidia tena. Nilitakiwa kukibadili haraka Kadri ya ilivyowezekana.

Nilikuwa nikiogopa kumuomba rafiki msaada kwani niliambiwa hedhi inapaswa kuwa siri. Nilidhani watu wangenishangaa kuwa kwenye siku zangu. Lakini niwaambie kitu wasichana wenzangu? Mama yangu amekuwa akiniambia Mara zote hofu ni hisia hasi juu ya jambo linalotarajiwa kutokea ila halijatokea bado hivyo kama ni naweza kuwa na mawazo hasi naweza pia kuwa na mawazo chanya.

Badala ya kufikiri watu watanishangaa kuwa katika siku zangu, nilijiambia kwamba hedhi ni kitu cha kawaida na rafiki wa kweli angefurahi kunisaidia. Kitu kibaya ambacho wangeweza kukifanya ni kukataa kunisaidia ila bado ingenipa nafasi na kuomba msaada kwa mtu mwingine. Sio jambo kubwa hivo, nilijiambia mwenyewe kimya kimya kama Mara 5 na kisha nikahesabu 5,4,3,2,1...na nilipofika 0 nikaamka kwenda kutafuta msaada. Nilimwendea rafiki yangu Asia na kumuomba pedi.

Kwa sababu si kuruhusu hofu kunizuia, niliweza kuongea na Asia na alinipa pedi 3 ambazo zingenisaidia kwa siku chache zilizofuata,na aliniambia kuomba pedi sio kitu cha kunifanya nijisikie aibu. Hakukuwa na haja ya kujificha pale unapokuwa kwenye siku zako. Hedhi ni jambo la kawaida katika hatua za ukuwaji, ni kitu cha kawaida kama vile kurefuka ama kuota nywele.

Asia alinishauri niwe natunza pesa ili niweze kununua pedi nitakazotumia na kuwa na chache za kuwasaidia marafiki watakaohitaji.

Baada ya kubadilisha pedi nilikaa kwenye chumba cha mtihani kwa furaha na kwa kujiamini. Ni nafurahi kwamba si kuruhusu hofu kunizuia. Wakati mwingine nitakapokuwa na shida sitajali kile watu wanachokifikiria. Nitakuwa jasiri na kuomba msaada Mara moja.

Share your feedback