Natamani kama nisingelikuwa nimemtumia
Mimi na Peter tumekuwa marafiki siku zote. Kila siku usiku huwa tunaongea kwa simu, Mara zingine kwa masaa kadhaa. Wiki chache zilizopita, aliniomba nimtumie picha zangu za utupu. Mwanzoni nilicheka na kumwambia 'haiwezekani' alianza kunitumia ujumbe wa sauti na kunibembeleza nimtumie. Nilizipuuza nikiamini ataboreka na kuacha.
Na siku moja nilipokuwa njiani nikitokea shule, aliniomba tushindane kukimbia. Aliniambia kama atanishinda, ningepaswa kumtumia picha yangu ya utupu. Sikuwa nimeshindwa bado hivyo nilikubali, lakini kwa namna moja nilikuwa nimeshindwa.
Nilimtumia picha yangu nikiwa nimevaa brazia ili kumnyamazisha. Lakini aliniomba picha nyingine ambayo nitakuwa nimepiga bila kuvaa brazia- akisisitiza alikuwa akinidai. Nilikubali na kumtumia picha nikiwa sijafunika nguo kwenye matiti yangu.
Nilijuta Mara tu baada ya kutuma picha Ile. Nilimuomba aifute, lakini alikataa kufanya hivyo. Nilichanganyikiwa sana, nilidhani alikuwa rafiki yangu.
Mama yangu alinigundua nimeanza kuwa mkimya na mwenye huzuni. Nilihofia kumueleza kuhusu jambo hili kwani sikutaka kumkasirisha.
Nilielewa kupitia mazungumzo tuliyokuwa tukiyafanya kuwa angependa nimuendee pindi ninapokuwa katika hatari yoyote au pale mtu anapojaribu kuniumiza. Hivyo niliamua kumuamini hata kama angeweza kukasirika kidogo, alikuwa ndiye mtu ambaye angeweza kunisaidia.
Nilimuuliza kama naweza kuzungumza nae kuhusu jambo binafsi. Nilimuomba awe mpole kwangu, kwani nilitambua kuwa nimefanya kosa. Alikubali. Nilipomueleza kilichotokea alishtuka na ilimvunja moyo sana, lakini alibaki kuwa mtulivu kama alivyoniahidi na tuliweza kufanya mazungumzo mazuri.
Aliniambia, pindi wasichana wanapopitia ubalehe, huwa wanapata umakini mwingi ambao sio sahihi kutoka kwa wavulana. Hata kutoka kwa wale tunaowadhani kuwa ni marafiki zetu wanaweza kutusukuma kufanya mambo ya kingono hata kama hatupendi. Alinieleza kuwa kuongea na watu ninaowaamini ambao wanaweza kukusaidia na kukupa ushauri ni jambo zuri mno Mara zote ninaposikia kusukumwa kufanya kitu.
Kwa pamoja tulizungumza namna mbalimbali za kukabiliana na swala hili. Alinisaidia sana.
Tuliamua kuzungumza kuhusu mambo mengi pamoja, na alinifundisha namna ya kuzizungumza hisia zangu za kuchanganyikiwa na za kukata tamaa. Hii ilinisaidia mno kumfanya aelewa kuwa kitendo alichokifanya kilikuwa kimeniumiza na alifurahi kuifuta Ile picha.
Natamani kama ningezungumza na mama yangu mapema- hakuna kitu asichoweza kukitatua.
Haijalishi ni mama yako, dada, rafiki au jirani - tafuta mtu unaweza kumuendea mambo yanapokuzidi.
Share your feedback