Lakini nilikuwa nimekosea!
Tumekuwa marafiki na rafiki yangu wa dhati Ana tangu siku ya kwanza shuleni. Nilikuwa na aibu kwa hiyo daima alinishika mkono na kunisaidia kuwa jasiri.
Karibia mwisho wa mwaka uliopita, Ana alianza kuwa tofauti. Kila wakati nilipotaka kutaniana naye – alikuwa anakataa. Alianza kukataa kila kitu nilichosema. Hata alianza kunishinikiza nisiende kutembea na marafiki zangu.
Nilifikiri labda alikuwa na wivu. Nilipata mpenzi na nilikuwa nimeanza kutengeneza urafiki na rafiki zake.
Ilikuwa inakaribia likizo na mpenzi wangu na marafiki kadhaa walikuwa wanapanga kwenda kununua chakula kwenye soko la usiku na kwenda kucheza mziki. Nilimualika Ana lakini alikataa – tena.
Tulianza kubishana. Nilimwambia nilikuwa nimechoka kujaribu kumualika kila wakati na anakataa. Nilikuwa niko tayari kukata tamaa.
Ana alianza kukasirika. Nilimwambia aniambie tatizo liko wapi na akaanza kuniambia kwa nini hakuwa anafurahia mimi kuwa karibu na kundi lile.
Ana alisema kwamba alikuwa amesikia uvumi kwamba kundi lile walikuwa wanakunywa pombe walipoenda matembezi. Hakutaka kujihusisha nalo wala hakutaka pia mimi nijihusishe nalo.
Sikuwa nafahamu kwamba kulikuwa na uvumi na nikamwambia Ana kwamba sikuwa nimeyaona mambo yale. Nilimuahidi kwamba ikiwa jambo hilo lingetokea ningemshika mkono na tuondoke pamoja papo hapo! Kama jinsi alivyonifanyia tulivyokuwa watoto.
Sasa ninajua kuwa muwazi kwa Ana na ninapoona mabadiliko katika tabia zake ninamwambia haraka iwezekanavyo – bila kukubali iendelee kwa wiki kadhaa.
Ana siyo rafiki mbaya, alitaka tu sote tusipatwe na matatizo. Ninafurahi sana tulizungumza na tuna uhusiano wa karibu kuliko awali!
Share your feedback