Kujifunza kuchagua marafiki wa kweli!

Na jinsi ya kuwaepuka walio bandia

Nilipoanza shule ya sekondari kidato cha tano niliwaacha marafiki zangu wengi na kujaribu kuingia kwenye kundi maarufu zaidi. Wasichana maarufu walionekana kuwa wenye furaha zaidi, walionekana zaidi na kamwe hawakuwahi kutaniwa wala kuonewa nilitaka niwe mmoja wao

Nilikuwa bado nina ukaribu na rafiki yangu kipenzi Zahra ambaye nilimjua tangu nilipokuwa mtoto, lakini tulizungumza kidogo shuleni. Marafiki zangu wapya hawakupenda mimi niwe karibu naye. Marafiki zangu wapya walikua wanavaa nguo tofauti tofauti na walijipodoa hatari hivyo nilianza kufanya hivyo pia. Niliacha kuwa kiongozi wa rika shuleni, kwani walisema hai kuwa poa na badala yake tulikutana tu kwenye egesho la magari baada ya shule.sikufurahia kama ambavyo nilitegemea.

Marafiki zangu wa zamani walisema kuwa nimebadilika sana, kwamba zamani nilikuwa mtu poa sana na kwamba sipaswi kuwasikiliza hao wasichana wengine. Sikutilia maanani ushauri wao, nilidhani labda walikuwa wananionea wivu tu kwa vile sasa hivi nimekuwa maarufu kuwazidi.

Siku moja asubuhi kabla yakwenda shule, mimi na marafiki zangu wapya tulikuwa dukani tukinywa juisi na Zahra akaja nje ya duka. Mmoja wa wasichana aliweka mguu wake juu na kumtega, ambapo ilimfanya Zahra kuanguka na kujimwagia juisi yake. Aliposimama alikua analia. Nilijisikia vibaya sana kwa ajili ya Zahra – Sikuweza kulivumilia jambo hilo kuendelea! Nilimsogelea nikamkumbatia na kumwambia angeweza kuvaa t-shirt yangu ya ziada ya michezo iliyokwenyebegilangu.

Niliwaambia wasichana ambao walimtega Zahra kwamba walivyofanya haikuwa sawa Kwamba kuwa muonevu kwa wanafunzi wenzako sio sawa. Na kwamba wanapaswa kutafuta mambo mengine ya msingi ya kufanya. Sikujali kama wangenichunia. Nilijua kwamba hili sio kundi la watu ambalo nilitaka kuwa marafiki nao tena. Hawakuwa marafiki zangu wa kweli.

Marafiki wa kweli husaidia, hukujenga, kukuwezesha kuwa toleo bora zaidi la wewe mwenyewe. Badala yake nilitumia miezi michache iliyopita kuwa toleo baya zaidi la mimi mwenyewe. Nilifurahi kumsimamia Zahra na nilijua kwamba angefanya vile vile kwangu. Nilikuwa na bahati sana kwamba marafiki zangu wa zamani walinisamehe, na sasa tuko karibu kuliko zamani.

Share your feedback