Ila hata sijali!
Siku zote nimekua na nyusi nyingii tangu nilipokuwa mdogo na hazijawai kunisumbua hata kidogo.Lakini siku hizi nazichukia kila ninapojiangalia kwenye kioo.
Unajua nini! nina umri wa miaka 14 na tangu nilipovunja ungo, mwili wangu ulianza kuwa na mabadiliko sana ambayo mengine sikuyapenda kabisa.Ninachopenda ni kwamba sasa hivi nina vimaziwa vidogo na nywele sehemu za siri na kwapani lakini sikupenda kuona vinyweleo vya usoni vinaongezeka na nyusi zangu kukua sana hadi kukutana katikati kama limdudu limekaa usoni kwangu.(ndo wenzangu wengi shuleni wananiambia hivyo)
Nimekua nikitamani sana kuondoa hivi vinyweleo vya usoni na kutafuta njia ya kuziweka sawa nyusi zangu,kwahiyo nilimfata mama kwa ushauri. Mama alikua muelewa na akanielezea kuwa wakati kubalehe ni muda ambao utapitia mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia na ni kweli wakati mwingine yanaweza kuwa mengi lakini unatakiwa kuvumilia ili uweze kuvuka salama, akaniambia kuhusu homoni na jinsi zinavyofanya kazi. Ni vitu muhimu katika mwili wako vinavyotuma taarifa ili kuusaidia mwili wako kupambana na vitu kama Njaa au hisia. Wasichana wanapopevuka miili yao hutoa homoni inayoitwa estrogen, na wavulana zinaitwa testosterone. Pia alinielezea kua tumeumbwa tofauti na miili yetu huitikia tofauti pale homoni zinapofanya kazi, baadhi yetu tunapata chunusi,hisia kubadilika,kujisikia huzuni au uchovu au hata kuota nywele za usoni kama mimi, akasema kufanya vitu vya kijinga wakati mwili wako bado unakua kunaweza kukuletea majuto badae.
Tukaongea kuhusu nilivyokua najisikia kutojiamini kwasababu wanafunzi shuleni walikua wananitania.Mamangu alinishawishi nijiangalie kwenye kioo na kisha akasema kwa sauti “Mimi ni mzuri jinsi nilivyo ndani hata nje”.Ilinisaidia kujisikia vizuri kuhusu mabadiliko ya mwili niliyonayo.Sasa hivi naurudia huu msemo kila siku asubuhi nikiwa najiandaa kwenda shule na imenisaidia kuelewa kua hizi nyusi zangu nyingi ni nzuri tu na ndio zinachangia kunifanya niwe wa kipekee.
Sasa hivi najisikia vizuri jinsi nilivyo,hata kama kuna mtu yeyote ananitania jinsi nilivyo ndo kwanza natabasamu na ninamwambia “Asante kwa kugundua jinsi nilivyo wa kipekee na mzuri”.
Share your feedback