Mwaka wangu wa kwanza kama Mama Ruthie

Nimekubaliana na yote!

Kuwa mama Ruthie kumekuwa ni kitu kizuri sana kilichowahi kunitokea maishani. Lakini ina changamoto zake,Ila poa tu sababu kila ninapofika nyumbani kutoka kwenye shule yangu uhasibu, huwa anakimbilia nyuma ya pazia, halafu ananiambia kwa sauti "Mama nitafute." Ina raha yake kwakweli kwa sababu vi miguu vyake huwa vinaonekana tu kweupee kwa chini ya pazia,Sikuwa nadhani kama itakuwa raha hivi, Siku hizi kila ninaporudi nyumbani huwa natamani tu kwenda kuona vi miguu vyake nyuma ya pazia.

Nilipogundua tu nimekuwa mjamzito nikiwa na miaka 16, nilichanganyikiwa na niliona maisha yangu ya baadaye yamejaa giza tu.Bahati nzuri Mama yangu alikuwa akinitia moyo niwe mama mzuri huku nikipambana kufanikisha ndoto zangu.

Mama, Ruthie na Nathan ambaye ni jirani yetu ndio watu wa muhimu zaidi katika maisha yangu. Sidhani kama ningekuwa hapa bila wao. Nakumbuka nilipotoka hospitali na Ruthie baada ya kujifungua katika zile wiki za mwanzo mambo yalikuwa magumu kiasi , lakini Mama aliniambia tutavuka tu mwanangu.

Mama alimwomba Nathanaongee na mimi kuhusu kusomea uhasibu.Siku zote nimekuwa mzuri sana kwenye somo la hesabu shuleni. Mwaka jana, kabla ya kumpata Ruthie, nilipewa zawa kwa kuwa mwanafunzi bora katika somo la hisabati darasani kwangu. Nathan ni mwalimu shuleni kwetu na alisema mimi nina kipaji. Nashukuru kwa yeye kuniambia yale maneno , sababu baada ya kumpata Ruthie, nilichanganyikiwa. Lakini cha kushangaza ni hiki kuwa, baada miezi 6 ijayo n ntakuwa nimehitimu.Yani sipati picha!

Sipati picha na mimi siku moja nitaitwa mhasibu! Nilisoma kwenye intaneti kuwa itabidi nisome kwa bidii ili nipate diploma, na nitakapohitimu nitafanya kazi kama mhasibu. Pengine hata siku moja nitafungua kampuni yangu ya uhasibu!

Mwaka jana nimejifunza mengi mno. Kwanza nimegundua ya kuwa mimi ni Jasiri, mimi ni mama mzuri kwa Ruthie, na pili naweza kufanya chochote ikiwa nitajiamini.

Share your feedback