Stori yangu ya hedhi yenye kuchekesha.

Kila mtu amewahi kupatwa na kitu cha kuaibisha

Mambo Springsters,

Nakumbuka siku niliyovunja ungo. Nilikuwa na miaka 12 nilikuwa na marafiki zangu tukifurahi bustanini siku ya jumamosi. Kila kitu kilikuwa kipo sawa mpaka pale nilipoanza kujisikia maumivu ya tumbo. Sikuona choo jirani hivyo niliamua kupuuza.

Maumivu yalizidi kuwa makali ikanibidi niamke na kuanza kumuuliza kila mtu anielekeze choo kilipo.

Rafiki yangu Emanuel aliniona nikiwa nimeinama huku nimeshikilia tumbo na akaniuliza kama nilihitaji kwenda chooni. Nilisikia aibu sana ila nilimuitikia kwa kutikisa kichwa kuonyesha kukubali. Ghafla alinibeba na kuniweka kwenye baiskeli yake na kisha tukaanza kutafuta choo kilipo pale katika Ile bustani. Hivi unaweza kuhisi nilivyokuwa nasikia aibu? Wakati mimi najisikia aibu karibia kufa Emanuel yeye anapiga kelele na kusema "choo, choo, tunataka choo".

Mpaka wakati nashuka kwenye baiskeli tayari nilikuwa nimekwisha chelewa. Nilichungulia kwenye suruali yangu na kuona tayari nilikuwa nimeanza hedhi! Kama ingenitokea kipindi cha nyuma ningesikia aibu mno na hata ningeweza kulia mno lakini sikufanya hivyo. Nimesoma stori nyingi sana kuhusu hedhi kutoka kwenye ukurasa wa Springster na ukweli ni kwamba hedhi ni kitu cha kawaida. Emanuel alinipatia sweta lake haraka ili nijifunge kufunika sehemu ilikuwa zimechafuliwa na damu. Hili sweta lilikuwa kubwa mno kwangu yani lilinivaa ikabidi tukauke kucheka maana nilikuwa kituko.

Niliingia chooni ili nikasafishe suruali yangu na kabla sijatoka nje kukabiliana na marafiki zangu wengine, nilichukua kitabu kutoka kwenye mkoba wangu kinachoelezea kuhusu kujiamini ni kitabu ninachokibeba Mara zote. Nilisimama mbele ya kioo na kuanza kusoma baadhi ya mistari ifuatayo yenye kutia nguvu.

  1. Hedhi ni kitu cha kawaida, sina sababu ya kusikia aibu.
  2. Maoni ya watu juu yangu hayawezi kueleza jinsi nilivyo. Mara zote nitajiamini.
  3. Mimi ni imara. Ninajiamini. Mimi ni mrembo.
  4. Ni kweli ninaweza kujisikia vibaya na kuaibika lakini hiyo haelezei vile nilivyo. Mimi ni imara. Nina jiamini. Mimi ni mrembo.

Nilirudia rudia kuyasema maneno haya mpaka pale ambapo wasiwasi wangu ulitoweka. Kuanza hedhi ukiwa kwenye sehemu za mikusanyiko sio sababu ya kukufanya usijiamini. Aibu ya muda mfupi haipaswi kudumu katika maisha yako yote. Jifunze kuipotezea na kujikita katika mambo chanya pekee.

Share your feedback