Lakini natamani kuishi kama jinsi nilivyo!
Wazazi wangu hunikosoa kila Mara. Hunikosoa kuhusu vitu kama vile kwanini napenda kuvaa t-shirt ndogo na kuvaa suruali "vimodo" , lakini mama yangu husema wasichana wanapaswa kuvaa sketi na magauni marefu. Lakini pia ananisema sana kuwa natumia muda mwingi kwenye kutumia simu yangu. Najisikia kama sifurahii maisha Kabisa
Baba nae amekuwa mkali sana kwangu. Napenda kutumia kompyuta na kujifunza kutengeneza programu, lakini hafurahishwi na swala la mimi kusoma masomo ya sayansi ya komputa. Alinifanya niachane na hilo somo mwaka huu.
Kaka yangu anaruhusiwa kula chochote, kuvaa na hata kufanya chochote anachojisikia. Jambo hili linaniboa sana.
Hivi karibuni mama yangu amekuwa akiwakosoa marafiki zangu, anasema haoni kama wananifaa. Eti hawana akili
Nawapenda marafiki zangu, Mara zote wamenisadia hasa kwenye kufanikisha safari ya ndoto zangu. Mama anasema wananipotezea muda na baba anasema sipaswi kuwa na marafiki wa kiume kwa umri wangu, kwani hii itapelekea watu kunifikiria vibaya. Nadhani hii hali imezidi sasa. Marafiki zangu wananicheka jinsi wazazi wangu walivyo wakali.
Wiki hii mwishoni kuna bethdei ya besti yangu kipenzi Lulu, na wazazi wangu wamesema siwezi kwenda na hawajanipa sababu yoyote ya kutokwenda.
Ninawaheshimu sana wazazi wangu kwani natambua wanajitahidi kunilinda, lakini pia natamani kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu mambo yanayohusu maisha yangu binafsi. Nadhani nimewathibitishia jinsi nilivyo muaminifu, hivyo naona wanapaswa wakubali tukae chini tuzungumze..
Niliamua kutulia kwa muda ili kushusha hasira na nilitaka kuzungumza nao wakati ambapo sikuwa na hasira hata kidogo. Nilipokuwa tayari, kwa utulivu kabisa niliwaambia najivunia juu ya mwanamke aliye ndani yangu, kwamba nilikuwa nikisoma kwa bidii na nilithamini urafiki wangu na kwamba nilitamani wanisapoti.
Niliwapa nafasi ya kutafakari na kusema kile walichokifikiria kiukweli waliheshimu mawazo yangu. Mwishoni mwa mazungumzo yetu wazazi wangu walivutiwa na jinsi nilivyoonyesha ukomavu. Wote walikubali kuunga mkono mawazo yangu.Na mama aliniahidi kutokuninunulia tena yale magauni mapana.
Share your feedback