Mawazo ya siri ya wavulana

Unataka kujua huwa wanawaza nini hasa?!

Mimi naitwa Salome. Nilipokuwa mdogo ilitubidi tuhamie mji mwingine ambako babangu alipata kazi mpya.nakumbuka jinsi nilivyokuwa naogopa kuhamia shule mpya, lakini nashukuru Mungu siku ya kwanza kila mtu alikuwa mwema kwangu na nkajikuta nimepata marafiki wengi sana.

Mmoja kati ya besti zangu shuleni. Anaitwa Adam.. ni kijana maarufu sana na humfanya kila mtu acheke. Mara nyingi utamkuta Adam anacheza kandanda wakati wa chakula cha mchana, , lakini huwa tunaenda nyumbani pamoja na tukipiga stori njiani na kucheza hadi jioni. Ni poa sana kuwa na rafiki mzuri kama huyu. Adam hunisaidiahomuweki zangu na huwa ananichangamsha ninapokuwa nimeudhiwa , na hunigawia chakula chake cha mchana ninapokuwa na njaa sana.

Siku moja tukiwa shuleni, Adam alinifata. Alionekana kuwa wasiwasi na alitaka tuongee faragha. Nilipoona tu uso wake nilipata hofu kwasababu kwa kawaida Adam huwa ni mchangamfu na mwenye tabasamu kila wakati.Hivyo kumwona akiwa siriazi kuliniogopesha. Nilimuuliza kuna shida gani? , alinieleza kuwa alipokuwa akitembea koridoni alimwona msichana aliyekuwa amekaa chini sakafuni peke yake. Msichana huyo anaitwa Yvonne ambaye ni mgeni hapa shuleni,na alionekana kuwa mpweke na Adam alitamani awe rafiki yake. lakini aliogopa kuanza kuongea nae.. Nikamshauri Adam ajaribu kuanzisha mazungumzo nae kwa utani ili kumchangamsha huku akimuuliza anajisiaje kuwa kwenye shule mpya. Nikamwambia asiogope, ma alivyo rafiki mzuri kwangu atakuwa rafiki mzuri kwa Yvonne pia ...

Hapo ndipo Adam aliponieleza kwamba wakaka wengi shuleni wanataka kuwa na urafiki na sisi wasichana kwa sababu sisi ni wajanja na wacheshi, lakini wakati mwingine wanaogopa sana kuongea na sisi. Nilishangaa sana kujua kwamba hivi ndivyo wavulana hutufikiria – Siku zote nimekuwa nikifikiri kwamba wanataka na kuwa marafiki na wavulana wenzao tu, lakini sasa najua wanawapenda wasichana pia!

Inafurahisha kuona kwamba hakuna tofauti kubwa ya jinsi wasichana na wavulana wanavyofikiri eh!

Share your feedback