Nitakuwa mjanja siku nyingine nitakapokuwa mtaani.
Siku moja jioni nilikuwa njiani nikitoka katika mizunguko yangu . Nilipokuwa nimekaribia nyumbani kwa mbele niliona kundi la vijana watatu wamesimama kwenye kona. Nilijua tu watanisumbua. Sikutaka kupunguza mwendo,na wala sikutaka kuwafanya wajue nilikuwa naogopa. na ilikuwa ngumu sana kurudi nyuma.
Hivyo nilichokifanya ni kuingia mtaa mwingine ili kuwakwepa. Lakini walikuwa wakinitazama huku wakinisubiri. Walivuka na kunifuata mtaa niliokuwa napita. Moyo ulinienda mbio. Niliogopa sana. Walianza kunipigia miluzi na kuniita majina ya ajabu ajabu. Waliniambia '' hebu njoo huku we mrembo, tutakufanya ufurahi" hakukuwa na mtu pale mtaani. kwa hiyo hakukuwa na mtu ambaye ningeweza kumuomba msaada. Nilitembea upesi lakini walikuwa wanaendelea kunifata nyuma yangu.
Nilipokuwa karibu na mojawapo ya kona za mtaani niliona moja ya duka likiwa bado lipo wazi. Nilikimbia haraka sana Kadri nilivyoweza na nikaingia dukani. Mara tu nilipoingia mle dukani nilianza kujisikia amani. Sikuwa pekee yangu kwani muuza duka alikuwepo pia. Nilimwambia "tafadhali naomba unisaidie, hapo nje kuna wavulana wananikimbiza" alitoka nje na kuwatafuta huku akiwaita lakini kumbe tayari walikuwa wamekimbia. Alimpigia simu Kaka yangu ili aje kunichukua na alikuja na nikafika salama nyumbani.
Kiukweli Hali hii iliniogopesha mno ila imenifunza mambo makubwa matatu :
Usitembee pekee yako nyakati za usiku. Mara zote jaribu kutafuta rafiki ambae anakuzid umri au hata mmoja wa watu wa Familia yako ili kutembea nae.
Epuka kupita mitaa isiyo na watu na ile yenye giza. Jaribu kupita kwenye mitaa iliyojaa watu ili usiwe mwenyewe.
Kuwa msafiri mjanja unaetumia teknolojia. Tumia simu yako kutuma au kuwapigia watu pale unapohisi upo katika hatari. Na unaweza kuwashirikisha watu mahali ulipo kwa kushea nao kupitia whatsapp ili wajue ulipo.
Kitu cha mwisho, unapokuwa mtaani usiwasikilize ama kujibizana na watu usiowajua wanapojaribu kusemesha au kukusumbua. Kama utajikuta kwenye Hali kama iliyonitokea mimi, usiruhusu uoga ukushinde. Fikiri kwa haraka na fanya maamuzi.
Share your feedback