Jinsi kufikiria kwa haraka kuliokoa mambo!
Ulikuwa usiku wa mwisho wa tamasha la maigizo na nilikuwa na furaha sana kwa onyesho la mwisho. Tulikuwa tunaendelea vizuri na nilipenda jukumu langu katika mchezo ule! Nilikuwa ndege aliyekuwa mjanja na mwerevu aliyemdanganya mwindaji na kuokoa ufalme wa wanyama. Nilipata hata fursa ya kupaa juu ya watazamaji kwa wakati flani , nikitumia kamba ngumu iliyokuwa imefungwa darini.
Saa moja kabla ya onyesho, nilianza kuumwa na tumbo. “Balaa gani tena hili limenipata,” niliwaza. “Lazima nimekula kitu kibaya.” Nilimeza dawa na nikaamua kupotezea.Nimekuja kwenye onyesho mimi.
Nusu ya kwanza ya onyesho ilikuwa nzuri sana, lakini nilipokuwa naingia kwenye jukwaa kwa tukio muhimu sana la onyesho - ambapo ninamdanganya mwindaji na kuwaokoa wanyama wote - nilihisi unyevu katikati ya miguu yangu. “Ah, hapana...” Nilifikiria, ghafla nikashtuka. “Nimeanza hedhi zangu.” Niligundua kwamba ilinibidi nifikirie haraka. Nilikuwa nimevaa nguo nyeupe na macho ya watu wote yalikuwa kwangu... Nkawaza fastaa nini cha kufanya!
Badala ya kupaa juu ya mwindaji na kuwaokoa wanyama, niliamua kudukia ndani ya chungu chake ili asinione..
Ingawa hii haikuwa sehemu ya Hadithi nilipigia kelele kwa wasaidizi wangu wa wanyama kutoka kwenye chungu. “Tafadhali nibebe hadi milimani. Lazima tuharibu chungu cha mwindaji kabla hajatufanya kuwa kitoweo!
Marafiki zangu walichanganyikiwa, lakini nilimkonyeza shoga yangu Sarah na nikamuonyesha sura ya huruma. Aliwaita haraka wasaidizi wa wanyama na wakanitoa jukwaani haraka. Nilipokuwa pale nilimwambia Sarah kwa haraka kilichotokea. Alinikumbatia na akaniambia nisiwe na hofu hata kidogo kwa sababu hedhi ni jambo la kawaida. Alinipeleka uani na kuwaambia wengine wafanye densi ya wanyama jukwaani. Alinipa pedi na sketi ya rangi ya pink nivae juu ya nguo yangu iliyokuwa na doa. Nilibeba mabawa yangu na nikakimbia jukwaani na kujiunga na densi ya mwisho ya kusherehekea.
Nashukuru Mungu kwa mawazo ya haraka na msaada wa shoga yangu niliokolewa kutoka kwa hedhi siku igizo na nikatumia ubunifu wangu kutokuaibika. Ninajivunia kufikiri kwangu kwa haraka na nina bahati kuwa na rafiki mzuri kama Sarah kunisaidia katika hali ngumu. Hedhi ni kitu cha kawaida na sio jambo la kuonea aibu!
Share your feedback