Ikiwa unalo wazo ila unashindwa kuanza kwa sababu hauna pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo.
Ikiwa unalo wazo ila unashindwa kuanza kwa sababu hauna pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo.
Huwa wanasema pesa huleta pesa-lakini wakati mwingine inaweza kuwa tofauti hasa pale unapotaka kuanzisha biashara unaweza ukaanza hata kama hauna pesa au una mtaji mdogo.
Yafuatayo ni mambo manne unapaswa kuyazingatia.
1. Tunza kidogo kidogo; je hauna pesa ya kutosha ili kuanzisha biashara yako, kuwa na subira. Njia rahisi ni kutunza pesa kidogo kidogo kila wiki au hata kila mwezi mpaka pale utakapopata pesa ya kutosha kuanzisha biashara, kwa kufanya hivi kutakuepusha kuingia kwenye madeni.Asilimia flani ya faida utakayoipata unaweza kuiongezea kwenye biashara yako ili kuisaidia ikue.
2. Angalia fursa zinazokuzunguka. Kama utaangalia kwa makini utagundua mara nyingi tunazungukwa na fursa kibao zinazoweza kutuingizia kipato cha ziada. Na unaweza kuanza kutunza kiasi hiki cha pesa utakachokipata ili kikusaidie kufungua biashara. Kitu cha kwanza kabisa unaweza kuwajulisha majirani zako kwamba unatafuta kazi ili kama watapata taarifa kuhusu kazi uwe wa kwanza kuambiwa.
3. Tumia ujuzi ulonao. Je umewahi kufikiria kuhusu kubadilishana ujuzi? Badala ya kuazima pesa au kununua kifaa chako binafsi, Angalia mazingira yanayokuzunguka. Yawezekana yakakuruhusu kubadilishana kitu kati ya muda, ujuzi na hata vifaa. Labda ngoja nikupe mfano; labda unahitaji cherehani ili kushona bidhaa unazohitaji kuziuza, unaweza kuazima cherehani kwa jirani yako na badala yake unaweza kuwaahidi kuwa utawasaidia kazi zao pale watakapokuhitaji kufanya hivyo.
Kitu cha kwanza ainisha ujuzi na vifaa unavyovihitaji ili kuanzisha biashara yako kisha omba msaada kwa watu wanaokuzunguka. Utashangazwa na jinsi unavyoweza kufanikiwa kirahisi pasipo kuhitaji pesa. Usiogope kuulizalabda wanaweza kukataa ila sio mara nyingi na siku zote watafurahia kukusaidia.
4. Tangaza biashara yako kwa njia ya kuambizana. Wanafamilia na hata marafiki zako ni njia nzuri sana ya kutangaza biashara yako. Waombe marafiki zako wawaambie marafiki na jamaa zao kuhusu biashara au huduma unazozitoa au hata wanaweza kukusaidia kutangaza kupitia mitandao yao ya kijamii. Mapendekezo binafsi kutoka kwa watu na pale wanapoizungumzia biashara yako vizuri itaisaidia mno kukua na kukuza jina lako na baada ya muda utashangazwa na jinsi taarifa zinavyosambaa haraka kwa njia ya kuambizana.
Kumbuka, sio lazima kuwa na pesa nyingi ndipo uanzishe biashara. Kuwa mbunifu, tazama fursa zinazokuzunguka,na tumia ujuzi na rasilimali walizonazo watu wanaokuzunguka ili kuanzisha biashara. Omba msaada kutoka kwa wanafamilia na marafiki ili wakusaidie kutangaza biashara yako nakwambia utashangaa jinsi utakavyofanikiwa pasipo kuhitaji pesa.
Share your feedback