Je unataka kuanzisha biashara?

Jifunze jinsi ya kushawishi watu!

Je, Umewahi kufikiria kuhusu kuanzisha biashara? Ikiwa umewahi, utahitaji kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi ili utoke kibiashara.

Kuanzisha biashara ni safari ndefu yenye milima na mabonde na sio kila mtu atakuunga mkono, ila wala usikubali hilo likakukuvunja moyo! Unaweza kubadili mitazamo ya watu ili kuwafanya wakuunge mkono katika safari yako kwa kujifunza kuongea nao na kuwashawishi.

Sabrina alitaka kuanzisha biashara ya kutengeneza mafuta ya nazi nyumbani na kuwauzia wateja wa nywele, lakini wazazi wake walitaka azingatie tu masomo yake shuleni. Alihitaji mkopo kutoka kwao ili kuweza kununua vifaa kwa ajili ya kutengenezea bidhaa zake na kutumia faida anayoipata kukuza mtaji.

Hivi ndivyo jinsi alivyopata "sapoti" ya wazazi wake na kupata Pesa!)

  1. Sabrina aliwaza kuhusu sababu zote zinazoweza kusababisha wao kupinga, na kubuni majibu kabla, hivyo alikuwa tayari kwa lolote,yaani Alijipanga. Mfano kwa hili ambalo, walidhani hiyo biashara yake lazima ingeathiri matokeo yake shuleni. Katika kuwajibu aliahidi kwamba ikiwa matokeo yake ya shule yatabadilika, basi atakuwa tayari kuacha biashara. #makubaliano

  2. Kisha, aliwaelezea jinsi ubunifu wake ungeleta manufaa kwake na kwa familia kwa ujumla. Mara zote, watu hufurahishwa na mawazo ,mazuri hasa kama yanawanufaisha wao pia.Hivyo, Sabrina aliwaelezea wazazi wake jinsi fedha zitakazopatikana zinavyoweza kusaidia kulipia kodi ya nyumba. Si hivyo tuu, pia itampa nafasi ya kujifunza mbinu zaidi ambazo zingemfanya kung’ara zaidi hata shuleni. #wazozuri

  3. Kuwaonyesha wazazi au walezi kuwa umeamua na uko tayari kufanya kazi kwa bidii itasaidia kuwashawishi ili kukusapoti katika malengo yako. Sabrina alikutana na changamoto fulani, lakini hakukata tamaa. alijaribu mara 20 kabla ya kufaulu kupata kile anachokitaka .Wazazi wake walikuwa wakiona jinsi anavyojitoa na uvumilivu wake katika kipindi chote.walivutiwa pia kwa kiasi cha fedha Sabrina alichoweza kutunza ili kuanzisha biashara yake.

Ilichukua muda lakini hatimaye Sabrina alifanikisha alichokitaka. Wakati wote kumbuka kuyakabili mambo kwa busara na kwa utii pale unapohitaji msaada. Usipopewa wala usikate tamaa, endelea kujaribu!

Share your feedback