Je imekuwa ngumu kupata Ajira?

Haya ni mambo matano ya kukusadia kujishugulisha

Huenda umemaliza shule na huna uwezo wa kuendelea na masomo zaidi hivi sasa. Na wakati huo huo unajaribu kupata ajira lakini imeshindikana.

Usihofu! Kutokuwa na ajira hakumaanishi ukae tu nyumbani. Wakati ukiendelea kutafuta kazi, unaweza kufanya vitu hivi vitakavyoweza kukusaidia kuandaa maisha yako ya baadae:

  1. Jitolee kufanya kazi katika shirika lililopo katika jamii yako. Kusaidia wengine huleta furaha ndani yetu. Jitahidi utumie masaa au siku chache katika wiki katika kufanya kazi ili uweze kutumia muda mwingi unaobaki katika kutafuta kazi yenye malipo. Kazi ya kujitolea huweza kuleta fursa na hukuongezea uzoefu utakaoweza kuuandika kwenye wasifu wako.

  2. Fanya mazoezi! Mazoezi ni njia nzuri inayoweza kuufanya mwili wako kuzalisha homoni zitakazokufanya kujisikia vizuri. Jiunge au anza darasa la mazoezi, Jiunge hata na timu ya michezo au kikundi cha riadha cha wasichana wengine walipo katika eneo lako. Hii ni njia nzuri ya kukutana na watu (Mmoja wao anaweza kuwa kukupa michongo ya kazi) na itakufanya ujisikie vizuri pia.

  3. Ikuze, iandae. Kieneo kidogo cha ardhi au hata kiboksi cha mbao chenye matundu kitakoni kinaweza kukusaidia kuanzisha bustani ndogo. Unaweza kupata mlo mzuri kiafya na kuhifadhi pesa. Na kama utakuwa na jitihada utaweza hata kuandaa chakula bora na kuwauzia watu ambao wapo bize na majukumu wanaoishi mijin ambao hawana muda wa kupika..Heiyaaa kibiashara change hichoo!.

  4. Jiunge na darasa. Tafuta darasa linalotolewa bure au kozi zinazotolewa kwa gharama nafuu. Kujifunza kitu kipya kunakusaidia kukua. Lakini pia ni njia nzuri ya kukutana na watu, hii kusaidia sana katika harakati za kutafuta kazi. Watu wengi hupata kazi kupitia watu wanaowafahamu. Kadri ambavyo watu wengi wanafahamu kuhusu swala lako la kutafuta kazi na ujuzi ulionao ndivyo ambavyo nafasi yako ya kupata kazi inavyoongezeka.

  5. Pata ushauri. Ongea na mtu ambaye anafanya kazi inayokuvutia, ili uweze kujifunza zaidi kuhusu kazi hiyo. Unaweza kuwatembelea kazini mchana ili kuona wanavyofanya kazi. Hii ni njia nzuri inayoweza kukusaidia kujua kama kweli hii ndio aina ya kazi unayotamani kuifanya.

Kutokuwa na kazi kunaweza kukufanya ujisikie mnyonge hasa pale ambapo kuna watu wanaokutegemea. Kuwa mwenye mawazo chanya na epuka kukaa na watu wenye mawazo ya kukatisha tamaa. Wale wanaokuahidi kupata pesa kirahisi au kwa njia za hatari ni watu wanaotaka kukutapeli tu. Tumia muda mwingi kuwa na marafiki wa maana na kufanya vitu vinavyokufurahisha. Hebu ipumzishe kidogo akili yako na mawazo ya kutafuta kazi kwa muda, hakikisha tu haupotezi muda.

Usikate tamaa ya kuizimiza ndoto yako kila la kheri.

Share your feedback