Kwa nini ni muhimu
Ukiwa na hela,huwa inakuwa rahisi kuzifanyia matumizi! Haswaa ikiwa kuna kitu ambacho umekuwa ukikitamani kwa muda mrefu – kama vile gauni,simu ya “Smartphone” au viatu fulani. Wakati mwingine kujinunulia kitu huwa si vibaya, lakini kutunza hela kwa ajili ya akiba ya baadaye ni muhimu sana.
Kuweka akiba, unapo pata pesa hata kama ni kidogo ni kitu kizuri sana kwa ajili ya maisha yako ya baadaye. Lakini mara zote huwa sio rahisi, Hivyo basi hii hapa ni namna ya kuanza.
Piga hesabu ya kiasi gani cha pesa unachohitaji sasa hivi – ikiwa ni lazima ununue vitabu vya shuleni au mahitaji mengine, kama dawa, ni sawa kutumia pesa. Kutoka hapo, unaweza kutenga pesa kidogo kwa ajili ya kujipa raha mwenyewe – labda kipafyum cha bei rahisi tu. Kiasi kinachobakia ndio utaweka kama akiba.Niweke shilingi ngapi? Fanya hivi wewe jaribu kuweka angalau nusu ya kile ulichonacho.
Zungumza na wazazi wako au mtu mzima anayeaminika kama shangazi kuhusu kufungua akaunti katika benki au kikundi cha kikoba mtaani. Baadhi ya vikundi vya kuweka akiba vinaweza kukuruhusu kufungua akaunti yako binafsi lakini vingine vinaweza kumruhusu mtu mzima tu akufungulie akaunti kwa niaba. Jambo zuri kuhusu kuweka pesa zako mbali hivi ni kuwa itakuwa mchakato mrefu wa wewe kuzichukua pesa zako na kuzitumia!
Ikiwa huwezi kufika benki, Basi unaweza tafuta kopo ambalo limekwisha tumika lilifungwa juu na chini na ukatoboa katundu kadogo kwa ajili ya kudumbukizia hela zako au unaweza kununua "kibubu" cha mbao au chenye funguo kabisa . ili hela zikae mbali kabisa na wewe.Waombe wazazi wako wakutunzie kibubu chako au hifadhi katika eneo salama ambako huwezi kukifikia kwa urahisi – hii itakurahisishia kutotumia pesa hovyo!
Kuweka akiba ni muhimukwa ajili ya maisha yako ya baadae– na ni tabia nzuri ya kuanza sasa kujifunza. Mambo mengi makubwa ambayo unatamani uyafanikishe maishani kama kusoma shule, kufungua biashara, kuolewa au hata kununua nyumba – yanaweza kugharimu pesa nyingi. Kwa kujifunza jinsi ya kutenga pesa sasa, itakuwa rahisi kumudu gharama kubwa za maisha wakati utakapofika.
Share your feedback