Je, Marafiki zako sio watu wazuri kwako?

Angalia ishara hizi.

Mawazo yako (10)

Kuna aina nyingi za watu katika ulimwengu huu, na sio kila mtu atakuwa mzuri kwako. Njia bora ya kupata marafiki watakaokufanya kuwa mtu bora zaidi ni kujifunza jinsi ya kuwatambua wale watakuangamiza..

Rafiki mbaya atakuchochea kufanya mambo ambayo hufurahishwi nayo.
Kwahiyo ikiwa hufurahishwi kuwa karibu na mtu fulani, au na kitu ambacho anakuambia ufanye, ni wakati wa kukataa.

Wanakukejeli wewe au kile unachokiamini.
Rafiki mzuri atakuheshimu hata kwa kile unachokiamini. Ikiwa mtu anakuhukumu, kukudhihaki au kukucheka kwasababu ya dini, sura au maamuzi yako ya maisha – mtu huyo hafai maishani mwako.

Hasikilizi unachokitaka.
Watu wenye mashauzi au waonevu siku zote hutaka uwasikilize bila kupinga wala kuhoji. Huenda ikawa vigumu kuwakabili, haswa ikiwa wewe ni mwoga. Lakini kama wanataka urafiki basi wanapaswa kujitahidi kukuhusisha na kusikiliza maoni yako.

Wewe mwenyewe hujisikii vizuri kuwa karibu nao.
Marafiki wazuri wanafurahia furaha yako. Jihadhali na watu ambao hawafurahii, wana chuki au wanazungumza mabaya kuhusu wengine – watajaribu kukufanyia hivyo pia.

Kumkataa rafiki mbaya kunaweza kuwa kugumu, lakini kunafaa. Ikiwa unataka kufaulu maishani, Andamana na watu wenye nia nzuri na wewe ambao watakusaidia kufanikisha ndoto na malengo yako.

Hebu tuambie, Je umewahi kuvunja urafiki mbaya? Tuandikie stori yako katika sehemu ya maoni hapa chini ili kusaidia wasichana wengine!

Share your feedback

Mawazo yako

kabix man lafik ndio anakuhalibiy mipang kabix yan

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nilikuwa sjui kwahiyo asante kwa kunijuza

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nilikuwa sjui kwahiyo asante kwa kunijuza

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

ni kweli hutokeaga hayo mambo unapokua na marafiki zako

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Latest Reply

Charney tunashukuru kwa maon yako. Je uliwahi kuvunja urafiki mbaya? Hebu tushikirike ili na wengine wajifunze. Asante

nikweli mm nilikuwa narafiki wakike sikujuwa kosaa nirilo vanya najuta kukosa rafiki wakike

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Kweli

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ndio

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Nilisha vunja Sana urafik

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ndio nimexhawahi kuvunja urafiki na rafiki yangu ambaye alikuwa akinixhawixhi kufanya vitu ambavyo nilikuwa xvipendi nikaamua kuachana nae ili kujenga malengo yangu ya baadae

Machi 20, 2022, 8:25 p.m