Kuwa makini na vitu vinavyozima ndoto zako.

Mambo haya 5 yanaweza kukuzuia usitimize ndoto zako.

Mawazo yako (3)

Dada mmoja mwenye hekima aliwahi kusema "kama unaweza kukifikiria kitu hakika unaweza pia kukitimiza" Mara zote huwa ni rahisi kuzungumza, lakini kinachosemwa ni kweli. Watu wote tunazo ndoto na malengo mbalimbali katika maisha ila sio wote ambao huyatimiza. Baadhi ya watu huishi kwa kujifunza na kutimiza ndoto zao wakati wengine hubakia na huzuni wakijilaumu kutokufanya maamuzi ya kutimiza ndoto zao.

Upo hai kwa makusudi maalumu, kila Msichana anao uwezo wa ubunifu ndani yake. Ubunifu huu pamoja na msaada kutoka kwa watu wanaokuzunguka, unaweza kuzifanya ndoto zako kuwa kweli. Hivyo kuwa makini na vitu tunavyooviita " Viua ndoto".

Baadhi ya vitu katika maisha vinaweza kukuzuia usiwe mtu uliyetakiwa kuwa, ama kuzima ndoto zako kabisa. Vitu hivyo ni kama vile

1. Uoga. Uoga ni namna ambavyo fikra zako hukwambia jinsi mambo yatakavyoharibika. Lakini kumbukeni kwamba sisi kama vijana tuna nguvu na uwezo wa kufikiri mambo yote yanaweza kufanikiwa. Hivyo badala ya kufikiria jinsi gani unaweza ukashindwa? Fikiri kuhusu namna unavyoweza kushinda.

2. Kutokujiamini Ujasiri ni ufunguo utakaoweza kukufanya kutimiza ndoto zako. Kutokujiamini kunakufanya uwe dhaifu na kukufanya ushindwe kutimiza lolote. Lakini kujiamini hukupa nguvu kubwa sana na hukupatia mafanikio.

3. Watu wenye Mawazo hasi sio kila mtu ataziamini ndoto zako. Watu wanaweza kukubeza lakini kamwe usiwasikilize. Cha msingi ni kuwa wewe mwenyewe unajiamini..Msichana pambana utimize ndogo zako. Usiwaruhusu watu wanaokuchukia wawe sababu ya wewe kutofanikiwa

4. Kutokuwa na msukumo wa ndani usiruhusu visingizio vikuzuie. Muda sahihi zaidi ni SASA. Msukumo utakuja mara tu utakapoanza na sio kabla (najua inaweza kuonekana kama kitu kigeni lakini ndio ukweli ulivyo) Kama ndoto zako zinaonekana kubwa sana basi anza na zile ndogo ndogo. Hatua ndogo ndogo zitakufanya kufanikisha mambo makubwa.

5. Vitu vinavyokupotezea mwelekeo Hiki ni moja ya vikwazo vikubwa sana, Je unakumbuka pale ulipotakiwa kufanya jambo kubwa lakini kuna vitu vikakupotezea mwelekeo na ukashindwa kulitimiza?

Ewaaa!,ndo huwa inakua hivyo hivyo, Ili uweze kuvizuia visizuie ndoto zako viandike na mara kwa mara uwe unavisoma. PiaWashikirikishe marafiki zako kuhusu ndoto zako ili muweze kusaidiana kuzitimiza

Hivyo mpaka sasa naamini umefahamu kuhusu vitu vinavyozima ndoto na jinsi ya kukabiliana navyo. Songa mbele na kamwe usirudi nyuma katika safari ya kuzitimiza ndoto zako!

Share your feedback

Mawazo yako

Asante Kwa Somo Zuri

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

je, ni siku gani huwa inaanza hedhi?

Machi 20, 2022, 8:25 p.m

Ni siku ipi hedhi hutokea?

Machi 20, 2022, 8:25 p.m