Je, unajua ukweli kuhusu dawa za kulevya na pombe?
Hebu fanya zoezi la kufurahisha ili utambue unajua ukweli kuhusu dawa za kulevya na pombe kwa kiasi gani
Maelekezo
- Utahitaji kalamu na karatasi
- Soma kila swali, kisha andika nambari ya swali na kisha jibu kama unaona ni NGANO au UKWELI, andika kando yake
- Bonyeza ukurasa unaofuata uone majibu
- Jumlisha idadi ya maswali uliyojibu kwa usahihi! Ili ufurahie zoezi hili zaidi lifanye pamoja na rafiki yako kisha mlinganishe majibu yenu
Maswali
- Pombe si mbaya kwako kama dawa nyingine za kulevya
- Usingizi unausaidia mwili kuondoa pombe
- Mwanamke mjamzito anayekunywa pombe anahatarisha afya ya mtoto wake.
- Kunywa kahawa hakumsaidii mtu kutokwa na ulevi
- Kunywa pombe hukufanya kuwa mwerevu
- Dawa za kulevya hukufanya kuwa mbunifu zaidi
- Kufadhaika ni dalili ya mtu aliye mraibu wa dawa za kulevya
- Kuvuta bangi huathiri jinsi unavyotembea au kukimbia na hufanya macho yako yasiweze kuona vizuri
Je, umepata ngapi? Bonyeza hapa ujue majibu yako!
Share your feedback