Je umeona jinsi sisi binadamu tulivyo tofauti? Kila mtu anapenda kuwasiliana na watu kwa namna tofauti. Baadhi yetu tunapenda kuchangamana wakati wengine wanapendelea kukaa peke yao muda mwingi. Hakuna anayekosea au kupatia lakini saa zingine watu wanatuchukulia vibaya kutokana na tofauti zetu.
Baadhi ya watu wanafurahi zaidi wakiwa peke yao. Wanapendelea kutumia muda wao kufanya mambo wanayoyapenda kama kusoma, kuangalia TV au kuchora. Tujibebe ipo hapa kukuambia kuwa hilo ni jambo la kawaida. Tunaamini kuwa ukiwa mtu mkimya au ukifurahia muda wako peke yako ina maana unafurahia kukaa peke yako na hakuna ubaya wowote kwa hilo!
Saa zingine watu hawalioni hili na wanaweza kuwa wasiowaelewa na wagumu hivyo hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kuwasiliana na watu kama unapenda kutumia muda peke yako:
Furahia utofauti wako: Tujibebe inajua kuwa hakuna jinsi sahihi ya kuwa au kutokuwa hiyo usijichukie kwa kujiangalia jinsi ulivyo badala yake zingatia uwezo wako ulionao wa kitofauti na kipekee. Onyesha wale walio karibu nawe mambo unayopenda kama kuchora, urembo na vipodozi au kusoma vitabu inaweza kusaidia kuafanya urafiki wako na watu kuwa imara na wa maana.
Zingatia uhalisia wako: kama rafiki zako wanakufahamu vizuri watajua kuwa hivi ndivyo ulivyo. Kuna nyakati unapenda kuchangamana; utataka kuongea nao na kuwasaidia lakini kuna nyakati unapenda kuwa na muda wako peke yako. Kuwaelimisha wenzio jinsi ulivyo unaweza mfuata rafiki mmoja kwanza ambaye unahisi atakuelewa vizuri na mwombe akusaidie kueleza kwa marafiki zako kuhusu uhalisia wako. Unapaswa kuwasiliana na watu katika njia inayoonyesha jinsi ulivyo kiuhalisia.
Sisitiza uwezo wako: Tafuta muda mtulivu na ufikirie mambo ambayo una uwezo nayo vizuri na unayoyapenda mwenyewe. Kisha unaweza kujaribu kuonyesha baadhi ya hayo mambo kwa rafiki zako, hii inaweza kuwa; kuchora kitu, kurekebisha kitu, kuwasaidia na kazi za shule, au hata kuwasikiliza ikiwa wana shida. Kwa kufanya hivyo itasaidia wale walio karibu nawe kufurahia utofauti wako.
Usijali. Wakati unajaribu kufanya haya yote kumbuka kutojichosha kufanya bidii kuwafurahisha wengine. Kwa kuwa uhalisi wako, utavutia wale ambao wataona uzuri ndani yako.
Mambo muhimu ya kukumbuka ni, kuwa wewe halisi, jua wewe ni nani na jiamini na utofauti wako. Sisi sote tupo tofauti na inabidi tufurahie utofauti wetu.
Share your feedback