Unda nenosiri bora

Kuzuia uvamizi kwenye akaunti yako.

Mpendwa Bi. Nai

Nilifungua akaunti yangu ya Facebook hivi karibuni. Rafiki yangu alinidokeza ya kuwa ninapaswa kuwa mwangalifu sana na nenosiri langu. Kuunda nenosiri salama kunamaanisha nini?*

Wako Mwaminifu, Teddy kutoka Mwanza

Mpendwa Teddy kutoka Mwanza,

Nenosiri ni kama neno ambalo ni kithibitisho chako katika kulinda taarifa binafsi ulizohifadhi katika simu ya mkononi au kompyuta yako. Ni kama ufunguo wa taarifa zote binafsi ulizonazo mtandaoni. Ni kama ambavyo usingependa mtu kuingia nyumbani kwako na kuangalia mali yako binafsi, humtaki mtu kuangalia taarifa zako binafsi mtandaoni.

Tovuti na simu nyingi za mkononi huhitaji nenosiri. Hii inaweza kuwa muunganiko wa nambari ya tarakimu 4 pia inayojulikana kama PIN, au linaweza kuwa nenosiri linalotumia nambari, herufi na alama.

Nenosiri salama ni muhimu sana unapotumia kituo cha huduma ya kulipia ya mtandao(internet cafe) au ikiwa unatumia simu moja na mwanafamilia mwenzako . Facebook na barua pepe yako vinapaswa kuwa na nenosiri tofauti. Usimpe mtu yeyote (Hata kama ni Besti yako) Ukiwa Intaneti kefu wakati unaingiza nenosiri kwenye kompyuta hakikisha unaziba ili watu wasione.

Unapounda nambari ya kuthibitisha au PIN chagua nambari 4 zinazomaanisha kitu maalum kwako, lakini ambazo zitakuwa ngumu kwa mtu mwingine kukisia. Kwa mfano, usitumie siku na mwaka wako wa kuzaliwa. Usitumie tarakimu nne za mwisho za nambari ya simu yako ya mkononi. Pia, usitumie nambari hizo nne, kama 2222. Aina hii ya msimbo wa kuthibitisha ni rahisi sana. Fikiria kitu cha ubunifu ambacho hutasahau kwa urahisi.

Unapochagua nenosiri, lenye maneno na alama fikiria kauli ambayo utaikumbuka kwa urahisi, lakini ile ambayo mtu mwingine hatakisia. Inaweza kuwa jina la kitabu au wimbo unaoupenda, na kila neno kwa herufi kubwa na nambari mwishoni. Kwa mfano: StoriYaNgu89. Pia unaweza kubadilisha herufi kwa alama, kwa mfano L@nGoLEtul@Jiji.

Epuka kutumia majina ya wanafamilia, marafiki, wanyama uwapendao, au chochote kinachohusiana na siku yako ya kuzaliwa, nambari yako ya simu, kijiji chenu au shule yako. Usiandike nenosiri mahali ambapo mtu anaweza kulipata kwa urahisi na kuingia katika akaunti yako.

Furahia unapounda nenosiri lako!

Mpendwa Bi. Nai

Share your feedback