Kubalehe... Kila mtu huipitia hatua hii!
Inawezekana umeshuhudia na kujisikia tofauti siku za hivi karibuni, baadhi ya sehemu katika mwili wako zinabadilika na umekuwa ukikwazika kirahisi. Haya yote ni mambo ya kawaida- huku kunaitwa kubalehe.
Kubalehe? Hebu nieleze zaidi...
Sote tumeumbwa tofauti ila moja ya vitu ambavyo tunafanana wote wavulana kwa wasichana ni kile tunachokipitia kipindi cha kubalehe. Hiki ni kipindi katika maisha yako ambapo inaonyesha sasa unaelekea utu uzima. Unaweza kuanza kubalehe mapema sana Kati ya umri wa miaka 7 au 8 na kipindi hiki huendelea kwa miaka Kati ya minne au mitano, lakini bado haijalishi ni lini utaanza kubalehe cha msingi ni kwamba watu wote hupitia kipindi hiki.
Muda wa mabadiliko
Vitu vingi vitaanza kuutokea mwili wako na unapaswa kufahamu yafuatayo...
Matiti yako yatakuwa
Utarefuka Zaidi
Nywele na ngozi yako vitakuwa na mafuta Zaidi
Mwili wako utaongezeka na umbo lako litakuwa bora Zaidi
Unaweza kuanza kupata chunusi
Utaota nywele makwapani na kwenye sehemu zako za siri
Utaanza kupata hedhi
Kile unachotakiwa kukifahamu kuhusu hedhi yako
Unapofikia kipindi cha kubalehe moja ya Kati ya mabadiliko muhimu sana katika mwili wa msichana ni pale unapoanza kupata hedhi.
Katika hatua za awali za hedhi yako, homoni zako zitafanya mayai katika ovari zako kukomaa. Hatua itakayofuata, ovari zako zitaruhusu mayai kutolewa. Wakati huo huo homoni zako zitausaidia mwili kutengeneza ukuta ndani ya tumbo lako la uzazi, ili kama mayai yako yatarutubishwa (na mbegu za kiume )kwa kujamiiana, basi ukuta uwe tayari kupokea mimba.
Kama mayai hayatarutubishwa, ukuta huu huondolewa kama kimiminika chenye mchakanyiko wa damu (hedhi). Hivi ndivyo ilivyo hakuna kitu cha ajabu ama cha kutisha, ni kwamba mwili wako unafanya mambo yake!
Kubalehe kunaweza kusemekana kama kitu cha kutisha hivii, lakini kumbuka kwamba watu wote hupitia hatua hii, hivyo tambua haupo peke yako.
Share your feedback