Na kipi sio cha kawaida?
Kupata hedhi yako kuna maana zaidi ya kutokwa damu kila mwezi kama sehemu ya maisha yako. Homoni zako huzifanya ovari na tumbo lako kufanya kazi, na huenda ukahisi hisia zinabadilika piaa. Huu 'mzunguko wa kila mwezi' unaweza kuchukua kati ya siku 21 na 40. Hapa kuna baadhi dondoo nzuri za kukusaidia ili kukupa ufahamu zaidi. .
Mayai ya mfuko wako wa uzazi yanaweza kukufanya upate kichefuchefu
Baadhi ya wasichana wengine wanaweza kabisa kulisikia yai likiwa linatolewa , katikati ya mzunguko wao wa hedhi. Unaweza kujisikia kichefuchefu kidogo na maumivu kiasi sehemu ya chini ya mgongo au tumboni. Unaweza hata kusikia kama kuna kitu kinakutoka mwilini,wakati yai linapotoka.
Maumivu ya tumbo
Ni kawaida wakati wa siku zako kupata maumivu ya tumbo au ile hali ya tumbo kukaza. Ukuta wa tumbo lako la uzazi hukaza kusaidia ukuta mwembamba kubomoka . Wasichana wengine huwa hawahisi chochote ila, wengine huhisi maumivu ya kuvuta, baadhi hupata maumivu yanayokuja na kupoa. Ikiwa ndio umeanza kupata hedhi, maumivu ya tumbo yanaweza kuwa makali mara ya kwanza, lakini huja kupungua baadae..
Kuwa mkali, Maumivu, Tumbo kujaa gesi, kuwa na chunusi , kukosa raha
Unaona kama Hedhi inakera eh? Hauko peke yako. Mzunguko wa siku zako unaendeshwa na homoni - estrojeni kwa ajili ya kuwezesha mayai yako kusafirishwa, projestroni kwa ajili kuandaa tumbo lako la uzazi. yaani hii inaweza sana kuathiri hisia zako. Ni kawaida sana kabla hujaanza siku zako hedhi yako, kujisikia hasira, kama ulie hivi, na kujisikia joto, kuwa mkali kupata maumivu mgongoni au chuchu kuuma, kutokwa na chunusi na tumbo kujaa gesi. Kula chakula bora, mazoezi kiasi, na kutumia dawa za kupunguza maumivu na kuoga maji ya moto vinaweza kusaidia.
Kuichunguza Chupi
Kila msichana yupo tofauti linapokuja swala la kinachotoka kwenye chupi zao - lakini maji ya uke au 'utoko' ni ya kawaida. Yanawezekana kuwa meupe au ya rangi ya krimu katikati ya mzunguko, au unaweza kupata madoa ya rangi ya kahawia kabla au baada ya hedhi yako (ni damu tu iliyochanganyika na oksijeni). Sio kitu cha kuonea aibu, wala cha kuogopesha.
Wakati wa kumuona muuguzi au daktari
-Kama unatokwa damu nyingi sana (kama vijiko 3-5 ni kawaida kwa kila hedhi).
-Ikiwa unapata madoa ya kahawia kwa muda mrefu
-Ikiwa unapata vidonda karibu na uke wako, utoko mzito, unaotoa harufu isiyo ya kawaida, wa kijani, njano au kijivu - haya yanaweza kuwa ishara ya maambukizi hivyo uwe na ujasiri na ukapimwe.
Share your feedback