Jifunze hapa kusimama tena baada ya kuanguka kwenye maisha.
"Hebu tuitengeneze kesho yetu leo na kuzifanya ndoto zetu kuwa halisi kesho"
Maneno haya yalisema na Malala Yousfzai mwenye umri wa miaka 18 ambaye pia ni mshindi wa nobeli ya amani (Nobel peace prize) na wakili wa haki za wasichana juu ya kupata elimu. Malala anakinzana na desturi mbovu na kuwa mmoja ya sauti zenye kuleta mabadiliko katika kizazi chake.
Stori ya maisha yake imewahamasisha wasichana wengi wadogo kusimamia kile wanachokiamini, na kufikia kilele cha mafanikio bila kujali ni mara ngapi wataangushwa na matokeo hasi.
Katika hatua zetu za maisha ya kila siku huwa tunafeli katika baadhi ya vitu. Lakini jambo la muhimu zaidi ni namna tunavyotazama kufeli huko! Je tuangalia kufeli kama mkosi au laana au utaamua kujifunza kutokana na makosa?
Hapa tunachagua kipengele cha pili. Njia nzuri ya kusimama baada ya kufeli au kukatishwa tamaa ni kujifunza kutokana na makosa. Fikiria , hivi ni kitu gani naweza kuboresha ili wakati mwingine nihakikishe napata matokeo mazuri ? Na nini kilisababisha hasa nikapata matokeo kama haya?
Hebu tazama dondoo zifuatazo ili zikusaidie kusimama tena pale utakapoanguka.
Kubaliana na matokeo. Ni kweli kwamba vitu havikwenda sawa na tulivyotarajia lakini tulijitahidi kutekeleza. Moja ya alama za washindi huwa ni kukubali makosa yao na kuyafanyia kazi kama funzo.
Tafuta kiini cha tatizo. Chukua muda kutambua kipi hasa hakikwenda sawa na ulivyopanga. Yawezekana haukutumia muda wa kutosha kusoma au haukupiga mahesabu ya matumizi vizuri. Mara tu utakapofahamu jinsi mambo yalivyoharibika itakuwa rahisi kuyarekebisha.
Fanyia kazi. Sasa kwa sababu unatambua nini hakikwenda sawa ni muda muafaka wa kuweka mikakati ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa wakati utakapopata nafasi nyingine. Iwe ni kuongeza muda zaidi wa kujisomea au kupinguza gharama za matumizi katika biashara yako- haijalishi ni kipi, anza kufanyia kazi taratibu ili kuzisogelea ndoto zako
Hamasika daimaEndelea kusonga mbele mpaka utakapopatia, kwani siku noja kila kitu kitakuwa sawa.
Acha kutoa visingizio Kuwa mkweli kwa nafsi yako kuhusu pale unapoteleza na utumie uzoefu huo kama njia ya kujifunza na itumie kama ngazi ya kupanda kuelekea kwenye mafanikio yako.
Je upo tayari kuanza kuzitimiza ndoto zako kama vile malkia kwa kujifunza kutokana na makosa? Songa mbele shosti.
Share your feedback
Mawazo yako
Sasa nazani ukianguka katika maisha hata katika masomo nivyema kutokatatamaa nivyema kuinuka na kuanza kupambana upya
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
nice
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
I learn dat no matter hw u face challenges In life BT when u accept those challenge and take on step forward this may cause u to reach ur goals and made ur future!!!βΊπππ
Machi 20, 2022, 8:25 p.m
Nice kwakweli nimeshawahi kupata chagamoto kama hiyo nilimaliza shule ya msingi sikufanya vizuli sana nikataka kulundia tena shule lakini sikufanikiwa nikaaa home kama mwenzi sita lakini anti akasema anakuja kunichukuwa tukakae arusha nikasema sawa nimekaa arusha mwenzi kama mitano nikaondoka kwenda dar nimekaa huko kama mwaka mmoja kwa kwa lafiki yake anti. Nilikuwa na fanya kazi za ndani ila hapo nilikuwa na ndoto yangu tuu ya kusoma nikwamwambia huyo dada kwamba nataka kusoma hakukataa akasema sawa nilianza kusoma shule za watu wazima nilisoma lakini huyo dada hakutaka me nisome aliazisha vulugu sana. Kunasiku nilienda shule nilipo Lundi home jion nilikuta maneno sana akaanza kunitukana sana half akanifukuza akaniambia nitoke nje na bengi langu la school sikukataa nikatoka nikamupigia ndungu yake momja hivi nikamwambia kuwa nimefukuzwa akasema nimusumbili anakuja nimekaa kidogo akaja akanichukuwa alipo nichukuwa nikaenda nae kwake nikaanza kusoma hivyo hivyo ila yeye alikuwa anakaa mbali sana na shule mpaka upande gara kwenda shule nauli nilikuwa sina ila alikuwa ananilipia namushukuru sana tumeenda ila na yeye alikuwa hana hata kazi ila alikuwa business humani maisha yalienda hivyo hivyo baada ya mda mfupi maisha yalitupiga sana nikawa siendi shule kwa sababu hela ya nauli hatuna me nikapotezea ila bado ndoto yangu ninayo sana ila maisha yametupiga sana nimeamua kuacha tuu sasa nipo tuu sina hata kazi nipo tuu ila nitakuwa sawa tuu nitafute hela kwanza shule nitaanza sun naombeni ushauli nifanye nn sasa
Machi 20, 2022, 8:25 p.m